RUTO KUUTETEA USHINDI WAKE MAHAKAMANI
Wanasheria wa Rais mteule nchini Kenya, William Ruto leo Agosti 26, 2022 mchana wamefika katika Mahakama ya Juu ya Milimani kupeleka vielelezo vya kutetea ushindi wa mteja wao kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9,2022 nchini humo.
Jopo hilo la mawakili limefika mahakamani hapo mchana likiwa na maboksi yenye viambatanisho vya kuthibitisha ushindi wa William Ruto uliotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya Agosti 15,2022.
Hii inatokea siku chache tangu aliyekuwa mgombea wa tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga kufungua kesi ya kupinga matokeo ya urais kwa madai ya kuwa mchakato wa uchaguzi haukuwa wa huru na haki huku kwenye madai hayo (petition) yakimuhitaji Ruto atoe vielelezo vya kutetea ushindi wake.
Ruto, ambaye tangu hasimu wake Raila Odinga afungue kesi mahakamani hajawahi kuizungumzia popote na badala yake siku ya jana Agosti 25,2022 akihutubia kwenye uapisho wa gavana wa Nairobi aliwapongeza wananchi wa Kenya kwa kumaliza ukabila nchini humo kwa kumchagua yeye na sio hasimu wake.
Comments