UMBALI WA KAYA CHANGAMOTO SENSA
Umbali wa kaya kwenye maeneo yanayokaliwa ya jamii ya wafugaji unachangia kasi kuwa ngodo ya uandikishaji kwa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi katika Halmshauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Haya yamebainishwa leo Agosti 28, 2022 na mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi katika wilaya hiyo, Nerbart Gavu alipokuwa akizungumzia maendeleo ya Sensa katika Halmshauri ya wilaya ya Chunya.
Amesema kuwa wameendelea na jitihada ya kuongeza makarani kwenye maeneo yaliyo na kasi ndogo ili kuhakisha kila mmoja anafikiwa.
Gvua amesema mpaka Jana Jumamosi kaya 59804 zilikuwa zimefikiwa na makarani katika Halmshauri hiyo huku akiwahakikishia wananchi kuwa wanafikiwa na makarani.
Amebainisha kuwa kata ambazo ziko pembezoni kuwa ni kata ya Kambikatoto, Ruaraje na Mafyeko na kueleza kuwa hali ya uhesabuji wa watu unakwenda vizuri kutokana na wananchi kuwa na uelewa wa kutosha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya sensa wilaya ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Chunya, Mayeka Mayeka amesema wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha uhesabuji wa watu unakwenda vizuri na kuwataka makarani wote wanaofanya kazi hiyo kuoongeza kasi ili kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa.
Comments