WAFANYABISHARA WAILILIA SERIKALI BARABARA YA MLOWO HADI KAMSAMBA

 



Wafanyabiashara na Wakulima Mkoani Songwe wametoa kilio chao kwa Serikali juu ya barabara ya Mlowo(Mbozi) hadi Kamsamba(Momba).


Wakiongea kwa nyakati tofauti wameizungumzia barabara hiyo ilio chini ya Tanroad's kuwa ni barabara kubwa kiuchumi hivi sasa na matumizi yake ni makubwa hivyo inahitajika kuangaliwa zaidi na Serikali kutokana na uhitaji wa barabara hiyo kuongezeka.


Kituo kikubwa cha mabasi na Daladala zitumiazo barabara hiyo kipo Mlowo Stendi Mpya ambapo asilimia kubwa ya magari yaliopaki humo ndani hutumia barabara ya Mlowo- Kamsamba.

Selina Nguku ni Mfanyabiasha wa Samaki ambapo amedai yeye usafiri kati ya mara mbili hadi tatu kwa wiki kuchukua samaki bondeni hivyo wamekuwa na changamoto kubwa ya barabara hiyo  amedai msimu wa Mvua huwa na tope na msimu wa jua Vumbi huwa ni kubwa na wakati mwingine hupelekea wao kuumwa.


"Hii barabara hivi sasa ni barabara ya pili kuiletea Uchumi Serikali baada ya Ile ya Tunduma,Mbozi inafuata hii Mbozi,Kamsamba Sasa sijui kwa nini Serikali haina hata Mpango wa kuijenga barabara kubwa namna hii" amesema Meshack Mkombe  mmoja wa abiria 


Wafanyabiashara wa Mabasi yapelekayo na kurudisha abiria Mlowo,Kamsamba yameiomba Serikali kuitazama barabara hiyo kwa jicho la tatu kwani wao kila siku wanalazimika kuyapeleka magari yao gereji kutokana na kuharibika mara kwa mara kwa magari yao.


Madereva wa Daladala za Mlowo,Itaka mpaka Mwanjelwa nao pia wametoa kilio chao na kuonyesha uchakavu wa Daladala zao maarufu kama Noa au punda wa Vumbi ambapo wamedai ongezeko la abiria ni kubwa na wao wanatoa huduma lakini hali ya magari yao ni mbaya yamechakaa.


"Tuna Wabunge wa Jimbo la Momba na Mbozi huwa hatuwasikii kabisa kulizungumzia hili na hata Viongozi wakija Songwe hawawapitishi barabara hii Sasa sijui changamoto za barabara hii watazijua lini" Filbert Mwakyembe


Idadi kubwa ya watoa huduma za usafiri barabara hii wanataka kujua Mpango wa Serikali dhidi ya barabara ya Mlowo,Kamsamba na wanashangazwa na ukimya wa Serikali na Viongozi wao hivyo wanaomba mikutano ya hadhara ya Viongozi wao wa Songwe na kuwataka wapunguze ziara na Vikao maofisini na kurudi katika kutatua kero za Wananchi Kwa kufanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero ambapo wamedai kuwaona Viongozi wakifanya mikutano ya hadhara badala yake wamekuwa wakionekana wakipita na misafara mbali mbali na tunaushia kuwaona kwenye Vyombo habari wakiwa kwenye Vikao Sasa sijui kero zetu watazijua vipi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE