Hii HAPA TOP 3 YA WABUNGE WACHAPA KAZI MKOA WA SONGWE
Mkoa wa Songwe ni miongoni mwa Mikoa ya mwisho kuanzishwa miaka ya hivi Karibuni Nchini Tanzania.Ikumbukwe Mkoa huu maarufu kama Lango la SADC ni Mkoa unaonekana kukua zaidi kiuchumi na Wananchi wake wanaonekana kujituma zaidi katika kujikuzia kipato chao.
Leo katika jamvi letu tumekuletea orodha na tathmini ndogo ya kituo hiki upande wa wabunge waliopo Mkoani humo.
Tuliamua kumuuliza Mwananchi mmoja mmoja na kuangalia utendaji wa Wabunge kwa Wananchi na umaarufu wao katika mitandao ya Kijamii katika mahojiano yetu Mbunge toka Wilaya mpya ya Songwe Mhe Philipo Mlugo anashika namba moja kwa kutajwa kama Mbunge ambae amekuwa jirani na Wananchi wake katika shughuli za kimaendeleo na muda mwingi hutumia Jimbo mwake na hata Shughuli nyingi za Kiserikali na chama Mhe Mlugo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kila kitu kina kwenda sawa.
Pia baadhi pia ya Wananchi wameizungumzia Mlugo kama Mbunge mwepesi kuwasaidia na kiufupi hana mkono wa birika.
Nafasi ya pili wamempa Mbunge wa Jimbo la Vwawa Japhet Hasunga na kumuelezea kuwa ni Kiongozi alieamua kujifunza tofauti na awamu yake ya kwanza kipindi chake cha awamu ya pili amekuwa jirani na Wananchi wake na katika maendeleo ya Jimbo lake na chama chake ambapo wamekwenda mbali kuwa Mhe Hasunga amekuwa mstari na mbele kujitoa na kuwapa usafiri pindi Wananchi wake wanapopatwa na misiba na hata Wananchi wanapompigia simu amekuwa mwepesi kupokea na kupanga nao mipango na kutatua.
Nafasi ya tatu wamempa Mbunge wa Jimbo la Ileje Godfrey Kasekenya amejitahidi sana kuibadili Wilaya iliokuwa gizani ya Ileje na sasa nuru ya kimiundo mbinu Wilayani humo imefunguka na amekuwa ni Mbunge wa kutekeleza na sio wa kufanya show za kimtandao.
Hawa ndio Wabunge watatu zetu tulizotaka kuzipata na hii ndio listi iliotajwa na tunajua Wabunge wote wanafanya kazi nzuri lakini si wote watakuwa sawa na tunatambua ukiwa Kiongozi lazima usemwe kwa mazuri na mabaya.
Haya ndio baadhi ya mambo yaliolalamikiwa zaidi na wadau tuliowahoji ikiwe baadhi ya Wabunge kutokuwa na mahusiano mazuri na Viongozi wenzao wa kiwilaya au Mkoa,kuendekeza Siasa za makundi,kutoshirikiana na Wananchi wao Katika shughuli za Maendeleo na wengine wamelalamikiwa kushinda zaidi mitandaoni na kujipost wakiwa katika matukio ya kibunge zaidi kuliko matukio ya kijimbo hivyo kuanza kukosa Imani kwa Wananchi wao.
Wiki Ijayo ungependa tuangazie upande upi wa Mkoa wa Songwe??
Tupigie 0679313119
Tafadhali tuachie maoni yako hapa chini
Comments