WAKAZI WA SONGWE WAOMBWA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO-19

 Mkuu Mkoa wa Songwe Mhe Waziri Kindamba amewataka Wakazi  Mkoani Songwe kuchanja chanjo ya Uviko-19 na kuachana na maneno ya kizushi kuhusiana na chanjo hiyo.

Kindamba ametoa rai hiyo katika Ibada ya swala ya Ijumaa iliofanyika katika msikiti wa Mkoa wa Songwe wa Masjid Nuur uliopo Wilayani Mbozi.

Akizungumka mara baada ya kukaribishwa na Sheikh wa Mkoa  Husein Batuza Mkuu wa Mkoa aliwashukuru na kujitambulisha rasmi kama Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliepata Uteuzi hivi karibu na kumbadili Mhe Omary Mgumba ambae amehamishiwa Mkoani Tanga.

Nae katibu wa Bakwata Mkoa wa Songwe ANNUARY ASHRAFF KHAN amewaomba Wakazi wa Songwe kumpa ushirikino Mkuu wa Mkoa Kindamba ikiwa na pamoja na kumsaidia kuzitangaza fursa mbalimbali za Mkoa huu




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA