PANYA ROAD 135 WAKAMATWA DAR


 Jumla ya wahalifu 135 wamekamatwa ndani ya siku nne jijini Dar es Salaam tangu kuanza kwa operesheni ya kuzia uhalifu iliyoanza Septemba 15, 2022.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amesema wengi waliokamatwa vijana wenye umri kati ya miaka 14 na 30 waliobainika kuhusika na matukio ya uvamizi mitaani maarufu kama Panya Road.

Makala amesema baada ya kuwakamata vijana hao walipohojiwa ilibainika viongozi wa magenge hayo baadhi yao waliwahi kutumikia vifungo mbalimbali magerezani.

“Nilitangaza Septemba 15 kuwa tumeongeza askari 300 lakini watu hawa hawakutaka kusikia wakaenda kujaribu kule Makongo na Ubungo.

Katika siku hizi nne, tumeweza kukamata vitu mbalimbali vya wizi vikiwemo runinga 23 na watuhumiwa 135 wamekamatwa wanaendelea na mahojiano.

“Wamekamatwa pia wanunuzi wakubwa watano wa bidhaa za wizi,” amesema Makala”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA