MAUAJI YA BODABODA WANNE MBARONI SONGWE

 W


ATU wanne wamekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Songwe kufuatia mauaji ya kijana Sadick Mwashambwa aliyechinjwa na watu watatu wasio julikana mbele ya mke wake akiwa na mtoto mchanga.

 

Kamanda wa polis Mkoa wa Songwe ACP Alex Mukama amethibitisha kukamatwa kwa watu hao wanne ambao hawakuwataja majina kutoka na na uchunguzi kuendelea kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea septemba 24 mwaka huu majira ya saa satano za usiku.

 

“Jeshi la polis mkoa wa Songwe linafanya uchunguzi wa tukio la mauaji ambalo lilitokea septemba 24, usiku katika kitongoji cha Kamficheni Kata ya Hasamba Wilaya ya Mbozi , ni kwamba Kijana Sadick Simiton Mwashambwa miaka 24 mnyiha  aliuawa na kushambuliwa na siraha yenye makali sehemu mbalimbali za mwili wake na kuchinjwa shingoni,

 

Watu wanne wamekamatwa tunawashikilia na  uchunguzi zaidi zaidi unaendelea “ alisema kamanda Mukama

 

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, mwenyekiti wa kitongoji cha Kamficheni Justin Ngondo ambaye naye inadaiwa kuwa anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi kwa kuhusishwa na tukio hilo alisema kutokea kwa tukio hilo, alisema siku ya tukio alipata taarifa kutoka kwa jirani wa marehemu na baada ya hapo aliwafahamisha wajumbe wa serikali ya kijiji ambao kwa pamoja walifika eneo la tukio na kujionea unyama uliofanyika.

 

“Mke wa marehemu ambaye kwa wakati mwingi alionekana kutokuwa sawa alitueleza kuwa wauaji wa mumewe walikuwa wanaume wawili na kwamba waliingia ndani kwa kuvunja mlango na baada ya hapo walimchinja mbele yake na kisha kutoweka bila kuchukua chochote” alisimulia Ngondo.

 

Alisema baada ya kukuta mwili wa marehemu ukiwa umechinjwa alichukuwa jukumu la kumpigia mtendaji wa kata Imma Simchimba ambaye aliwataarifu polisi.

 

“Baada ya polisi kufika na kufanya uchunguzi, mwili wa marehemu licha  ya kuchinjwa pia mwili wake ulikuwa umekatwa katwa na kuwa na majeraha mengi”.

 

Akizungumza huku akiwa katika hali ya majonzi makubwa shangazi wa marehemu, Lydia Mwashambwa alisema walipokea taarifa za mauaji ya shangazi yake usiku wa tukio na kufika ambapo walikuta mwili wa marehemu ukiwa umechinjwa katika hali ya kinyama.

 

Alisema siku moja kabla ya tukio aliongea na marehemu na kumueleza kuwa ameachana na kazi ya Bodaboda.

 

“Juzi alikuja nyumbani akanambia kwa sasa nimeacha kazi ya Bodaboda nimeanza kufyatua tofali mbugani…sasa sijui ni kitu gani kilitokea na kumfanyia mauaji mwanangu” alisema shangazi wa marehemu huku akibubujikwa na machozi.

 

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya serikali ya Vwawa, Wilayani Mbozi, Dkt. Kenneth Lesilwa, alithibitisha kupokea mwili wa marehemu wa tukio hilo na kwamba tayari timu ya wataalamu imefanyia uchunguzi na kwamba walikuwa wakisubiri kuwakabidhi ndugu.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE