JE WAJUA MKOA WA SONGWE UMEJIANZISHIA VAZI PENDWA LA TAIFA??


 Staili ya kuvaa bangili za shanga au nyuzi mkono wa kulia zenye rangi ya bendera ya Taifa imeonekana kupamba kasi ndani ya Mkoa wa Songwe.


Mamia ya Wakazi wa Mkoa wa Songwe wameonekana katika mkono wao wa kulia hivi sasa wakivaa bangili hizo zilizonakishiwa na shanga au nyuzi zenye rangi ya bendera ya Tanzania.


Asimilia kubwa ya Vijana wa kike na wakiume wameonekana Mkoani humo wakiwa katika vazi hilo.


Mwandishi wetu ambaye pia ni mwanachama au kipenzi wa kuvaa Vazi hilo linaloshika kasi kwa sasa aliamua kuwahoji baadhi ya Watumishi Mkoani Songwe hususani walio katika Ofisi za Mkoa wa Songwe ambapo walifunguka huku asilimia kubwa wakiombwa wasitaje majina.

"Mwandishi tusikudanganye Katibu wetu Tawala Happiness Seneda ndio katuhamaisha hapa ofisini na ukimuangalia mkono wake wa kulia ana vazi hili hivyo tumejikuta tu nasi tunahamasika kuvaa na mpaka sasa tunaona asilimia kubwa ya Wananchi wa Songwe imekuwa kama vazi rasmi na kiukweli huu ni uzalendo wa hali ya juu kuona Watanzania wanahamasika kuvaa vazi lilonakshiwa na rangi za bendera ya Taifa" amesema mmoja ya Makatibu muhtasari wa Mkoa.


Baadhi ya Wananchi Mkoani Songwe wameonyesha kupendezewa na Vazi hilo ambapo wao wamesema kuwa Nchi Sasa imepata Vazi lake la Mkono kilichobaki ni Mamlaka husika kuitangaza uwepo wa vazi hilo na huvaliwa Mkono wa kulia.


Lakini pia wengine wameomba hamasa zaidi ifanywe na Viongozi ngazi ya Mkoa kuhamasisha makundi mbalimbali yawe Wazalendo kwa Nchi yao na jwa kuwa Vazi hilo la Mkononi limependwa basi lihamasishwe zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE