RC TANGA AAGIZA WATUMISHI WANNE WASIMAMISHWA KAZI
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba ameagiza kusimamishwa kazi watumishi wanne wa Halmashauri ya Muheza kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo.Pia, ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuwahoji watumishi hao.
Mgumba ametoa maagizo hayo leo Jumatano Oktoba 19, 2022 wakati wa ziara yake wilayani Muheza ya kukagua miradi ya maendeleo.Pia, ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuwahoji watumishi hao.
Mgumba ametoa maagizo hayo leo Jumatano Oktoba 19, 2022 wakati wa ziara yake wilayani Muheza ya kukagua miradi ya maendeleo kusimamishwa kwa watumishi hao kumekuja ikiwa ni mwezi mmoja na siku 19 kupita tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nassib Mmbaga kusimamishwa kazi na aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo na utendaji kazi usioridhisha.
Watumishi hao waliosimamishwa ni Ramadhani Mtingi (Idara ya ujenzi), Zainabu Mzindakaya, Mweka hazina wa Halmashauri (DT), Furaha Sarakikya Idara ya Manunuzi na Ofisa Elimu Sekondari, Serapion Basgange, Mwanasheria wa Halmashauri ya Muheza, Aisha Mhando na Meneja Mradi wa Abdallah Hasani.
"Tunaanzia na hawa wa nne na wengine kadri ninavyopata taarifa nitatoka na maelekezo na hawa sio wasimame kupisha uchunguzi maalumu lakini pia Takukuru uanze kuhangaika nao" ameagiza Mgumba
Pia, ameagiza Mkazi wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi maalumu kwa miaka mitatu mfululizo katika miradi yote ya maendeleo Wilayani humo.
Kwa upande wake Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Zainab Bakari amesema kuwa amepokea maelekezo hayo akiahidi kuyatekeleza.
Comments