MTOTO AUWAWA WAKATI AKICHUNGA NG'OMBE

 MTOTO wa Miaka 10 kutoka Kijiji cha Kakese Kata ya Kakese Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ameuawa na watu ambao hawajatajwa majina wakati akiwa kuchunga Ng’ombe.

 

Akiwa katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kakese kata ya Kakese, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24,2022 wakati Mtoto huyo akiwa machungoni na ndipo alipokutana na watu hao wenye lengo la kuiba Ng’ombe wanne waliokuwa wakichungwa na Mtoto huyo.

 

“Pengine aliwatambua na wenyewe wakamtambua kwa hiyo wakaona ili kufanya namna gani iishe ni kufanya ukatili kwa kiumbe kile”

Wananchi wa Wilaya ya Mpanda katika Kata ya Kakese wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Jamila Yusuph

Hata hivyo,DC Jamila amesema Ng’ombe hao wamepatikana na wahusika wote wamekamatwa.

 

DC Jamila ametoa pole kwa familia iliyokumbwa na kadhia hiyo huku akiwaahidi Wananchi kuwa Serikali itaimarisha ulinzi na wote wanaovunja sheria watachukuliwa hatua.

 

Kwa upande wao Wananchi wa Kijiji hicho wameililia Serikali kuona namna wanaweza kujengewa kituo cha Polisi kwani usalama Kijijini hapo umekuwa mdogo kutokana na wizi kushamiri vikiwemo vitisho.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE