RC ATAKA DC NA DED KUJITAFAKARI FEDHA ZA MIRADI


 Na Ibrahim Yassin,Rukwa


MKUU wa mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amemtaka mkuu wa wilaya ya Kalambo, Tano Mwera na Mkurugenzi wa halamsahauri hiyo, Shafii Mpenda kujitafakari kutokana na kushindwa kukamilisha kwa wakati miradi ya afya inayotekelezwa wilayani humo.

 

Agizo hilo amelitoa Jana kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya afya inayotekelezwa wilaya humo pamoja na kuongea na wananchi ili kusikiliza na kutolea majibu kero zinazo wakabiri.

 

Sendiga alisema kuwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya vituo vya afya ambavyo ni kituo cha afya Kanyezi kinachojengwa kwa thamani ya sh. Milioni 400, Legeza Mwendo kinachojengwa kwa thamani ya sh.Milioni 700 lakini bado havijakamilika.

 

Alivitaja vituo vya afya vingine kuwa Mwazye kinachojengwa kwa sh. Milioni 500 pamoja na hospitali ya wilaya ya Kalambo inayojengwa kwa sh. Bilioni 3  ambavyo kwa pamoja vimeshatumia zaidi ya shilingi Bilioni 4.6 lakini huduma bado hazijaanza kutolewa.

 

Alisema kuwa ujenzi wa vituo vya afya ulianza tangu mwaka 2018 ni miaka mitano sasa haujakamilika na serikali imekua ikitoa fedha ambapo amebaini kuwa tatizo ni viongozi na watendaji wa serikali ya wilaya hiyo kutosimamia miradi hiyo vizuri.

 

“Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi lazima mkae chini na kujitafakari wilaya hii ina shida gani?, Kalambo kuna shida kubwa  miradi haikamiliki kwa wakati....Siwezi kukubali kuona miradi yenu inakwama wakati wananchi wanahitaji huduma” alisema.

 

Mkuu huyo wa mkoa ametoa siku kumi na nne kwa viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe huduma za afya zina anza kutolewa kwenye vituo hivyo vya afya wilayani Kalambo ili wakina Mama wajawazito na watoto wapate huduma karibu na maeneo wanayoishi.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Sunday  Wambura inaonesha kuwa  vituo hivyo vilianza kujengwa mwaka 2018 na mpaka sasa ni miaka mitano lakini haijakamilika na huduma bado hazijaanza kutolewa.

 

Naye Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Legeza Mwendo, Emmanuel Matinda alisema changamoto kwenye miradi hiyo ya afya ni upatikanaji wa fedha za ndani za halmashauri ili kukamilisha kazi ndogo kama mifumo ya maji taka, umeme na jengo la upasuaji ili huduma kwa wananchi zianze kutolewa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE