BREAKING NEWS:WATU ZAIDI YA 54 MBOZI WADAIWA KUDHULIKA NA POMBE YA KIENYEJI,MUUZAJI WA POMBE AFARIKA DUNIA

Wakazi zaidi ya 45 Katika Kijiji cha Nambala kilichopo kata ya Mlowo Wilayani Mbozi wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi baada kudaiwa kunywa pombe ya kienyeji ambayo mpaka sasa chanzo chake cha kudhulika bado kinachunguzwa na jeshi la Polisi.


Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Mbozi Kenneth Lesilwa amesema wao kama hospital ya Wilaya wamepokea waathirika wa pombe hiyo zaidi ya 54 na maiti moja ya Muuzaji wa Pombe aliefahamika kwa jina la Kenneth Nzunda 57 mkazi wa Nambala ambae yeye alikuwa anajihusisha na uuzaji wa pombe za kienyeji.


Mganga Mfawidhi amesema jana majira ya saa sita Mchana walipokea waathirika idadi yao kwa ujumla 45 na watano kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.


"Marehemu Kennedy Nzunda ndie aliekuwa muuzaji wa pombe hiyo yeye alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika moja ya hospitali binafsi Wilayani Mbozi na aliletwa hapa akiwa tayari ameshafariki na katika hospitali hiyo binafsi kuna waathirika wengine sita hiyo jumla yake wapo 54"Amesema Mganga Mfawidhi.


Kwa upande wa jeshi la Polisi Kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe ACP Alex Mkama amesema jeshi la Polisi limetuma wataalamu katika Kijiji hicho cha Nambala Ili kuweza kujua chanzo halisi cha watu kuathirika na pombe hizo


"Nitoe wito Kwa Wananchi kuzingatia usafi na usalama wa Vyakula na Vinywaji wakati wakuviandaa Ili kuepuka madhara yanayoweza kuambatana na Mazingira machafu.


Habari kutoka kwa wakazi wa Kijiji cha Nambala wamedai pombe hiyo ilikorogwa na Siwema Mwampashi (40) anedaiwa ni Mke mdogo wa Marehemu Kennedy Nzunda

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE