UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk Festo Dugange amesema takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano bado ni kikubwa ambapo kwa Mkoa wa Kigoma ni asilimia 27.1, Katavi asilimia 32.2, Njombe asilimia 50.4, Songwe asilimia 31.9 na Rukwa asilimia 49.8. Amesema hayo katika hafla ya kusaini hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa lishe unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) iliyofanika leo Mei 07, 2024 katika Ukumbi wa Sokoine jijini Dodoma. Dk Dugange amesema viwango vya matatizo ya lishe nchini vimeendelea kupungua mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2022 kiwango cha udumavu nchini ni asilimia 30 ikilinganishwa na asilimali 34 mwaka 2015. Aidha, naibu waziri huyo amesema tunapaswa kuendelea kuhamasisha ulaji wa chakula mchanganyiko chenye virutubisho na kuzingatia mtindo bora wa maisha. “tuweke kipaumbele katika kuimarisha usafi wa mazin...



Comments