KATIBU TAWALA SONGWE SENEDA AWAPONGEZA JUMUIYA YA KIISLAMU MKOA WA SONGWE KWA WAZO LA KUANZISHA CHUO CHA MAADILI
(Katibu Tawala Mkoa Songwe Happnes Seneda)
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Hapness Seneda amehudhulia Sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Saw) Maulid iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa kiisalamu Mkoani Songwe katika msikiti wa Ijumaa wa Noor uliopo Vwawa Wilayani Mbozi.
Sherehe hiyo iliofanana kwa kaswida na usomaji fasaha wa Quruani ilienda sambamba na Nia ya kuanzishwa cha Chuo cha mafundisho ya Dini na maadili (Madrasa) Ili kuweza kutoa mafunzo Kwa Watoto wa kiisalamu pamoja na dini zingine.
(Wanawake wa Kiisalamu Songwe akiimba na Kupiga madufu katika Maulid ilifanya Mbozi)Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiisalamu Mkoani Songwe Bi Tatu Ramadhani amesema Jumuiya hiyo imekuja na wazo la kuanzishwa Chuo hicho Ili kuwafunza Watoto maadili ya Dini na kuwaepesha matendo ovyo ya Dunia na kujenga kizazi chenye hofu na Mungu na Maadili mema.
Aidha amesema Chuo hicho kitawafundisha Watoto wote bila Kujali Dini wala jinsia hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia kwa hali na mali Ili kuweza kufanikishia wazo la Jumuiya la kujenga Chuo hicho.
Kwa Upande wake Katibu Tawala ameipongeza Jumuiya hiyo ya Wanawake wa Kiisalamu Kwa kufanya Maulid pia kwa kuja na wazo la kuanzishwa Chuo cha mafundi ya Dini na Maadili na Jumuiya hiyo.
Seneda amewapongeza na kusema kitasaidia kuijenga Jamii yenye Maadili na kuepusha mmong'onyoko wa Maadili Nchini Tanzania
"Tukiwa na Chuo Kwa aina hii pia Wazazi tukionyesha ushirikiano kwa kuwapeleka Watoto wetu itasaidia sana kuwajengea Watoto wetu au kuijenga Jamii yenye Maadili mema na hofu na Mungu hivyo itapunguza changamoto hii tulionayo sasa ya Watoto wetu wengi kukosa Maadili na kujiingiza katika Vitendo visivyofaa" amesema Katibu Tawala Seneda.
Comments