MIL,300 ZA SERIKALI KUU ZIMETUMIKA KUJENGA NYUMBA YA MKURUGENZI WILAYA YA SONGWE


Na Rahim Secha,Songwe


ILI kuhakikisha tatizo la nyumba za watumishi lina malizika serikali imetoa Ths,Milioni 300.000.000. kujenga nyumba ya kurugenzi katika halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani hapa hali itakayopunguza tatizo la nyumba za watumishi.


Wilaya ya Songwe ni moja ya halmashauri mpya mkoani songwe iliyomegwa kutoka wilayani Chunya mkoani Mbeya miaka kadhaa iliyopita ikiwa na changamoto nyingi kutokana na upya wake hasa uhaba wa nyumba za watumishi.


Uhaba huo wa nyumba za watumishi umeanza kufanyiwa kazi baada ya serikali kuu kutoa kiasi hicho cha Tsh,Milioni 300,kujenga nyumba ya mkurugenzi ambapo nyumba zingine za watumishi zikiwa zinaendelea kujengwa hali inayochochea hamasa ya utendaji kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo.


Mzee Ayoub Mwashilindi mkazi wa Mkwajuni alisema yeye ni mzaliwa wa wilaya hiyo tangu ikiwa sehemu ya Mbeya,kulikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ofisi na nyumba za watumishi,lakini kwa awamu hii alisema ameona kasi ya ujenzi wa miradi mbalimbali Pamoja na nyumba za watumishi.


Alisema ana kila sababu ya kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutambua umuhimu wa kuijenga wilaya hiyo ambapo kwa sasa kila sekta imefanyiwa maboresho huku miradi zaidi ikianza kujengwa na kwamba anaipongeza serikali kwa kutambua umuhimu huo.


Akizungumza leo  katika ukaguzi wa mradi huo,kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, fransisca Nzota, alisema halmashauri ya Songwe inatekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba hiyo kwa Tsh,Milioni 300 kwa awamu ya kwanza walipokea Ths,Milioni 150 na kiasi kilichobaki kimewekwa kwenye bajeti yam waka 2022-2023 kwa ajili ya umaliziaji.


Alisema ujenzi huo ulianza mwezi Machi 2021 hadi 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 30 mwaka 2022 ambapo kwa sasa upo asilimia 70.


Aidha Nzota,alisema kumekuwepo kwa changamoto ya uchelewaji wa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi huo,na kwamba utakapokamilika utaboresha mazingira ya kuishi mkurugenzi.


Katibu tawala mkoani Songwe,Happiness Seneda,alisema kutokana na umuhimu na kutambua mchango wa watumishi katika utekelezaji wa shughuri za maendeleo,serikali imetoa Kiasi hicho cha Fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo huku nyumba zingine za watumishi zikiendelea kujengwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE