MILIONI 90 ZA SERIKALI YA MAMA RAIS SAMIA ZIMETUMIKA KUJENGA VYUMBA VIWILI VYA MAABARA SHULE YA SEKONDARI SUME -SONGWE
Na Rahimu Secha,Songwe
WANANCHI wa vijiji vilivyopo kata ya Mkwajuni wilayani Songwe mkoani hapo wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu kwa kutoa kiasi cha Milioni 90kujenga nyumba viwili vya maabara Pamoja na thamani zake hali itakayosaidia wanafunzi kujifunza masomo kwa vitendo.
Awali shule hiyo ilikuwa haina maabara hali iliyowapa changamoto wananfunzi kujifunza kwa vitendo hasa masomo ya fizikia na sayansi ambapo kwa sasa changamoto hiyo imetimizwa baaada ya serikali kusikia kilio cha wananchi.
Mayasa Msafiri mkazi wa Mkwajuni,alisema licha ya wao kuwa na muamko wa kuwapeleka shule Watoto wao lakini walikuwa wakikabiliwa na ukosefu wa maabara ambapo kwa sasa ujenzi wa maabara za kisasa zipo hatua za mwisho huku akiwa na uhakika wanafunzi wataongeza ujuzi mara dufu kwa vitendo.
Hayo yalifanyika leo katika ziara ya kikazi ya katibu tawala mkoani Songwe akiwa wilayani humo ambaye alizungumza masuala mbalimbali ya kielimu na kuwataka wazazi kuwapeleka Watoto wao shule ili wapate haki zao za kimsingi.
Afisa elimu sekondari wilayani humo,Stephen Bange alisema mradi huo umekamilika kwa ngazi ya msingi,yaani kuta,kuezeka na kupaua Pamoja na upigaji wa dari,madirisha Pamoja na mambo mengine ikiwemo mifumo ya maji ambapo kiasi cha Milioni 90 kimetumika ambapo halmashauri imechangia Ths,19,0270,00 kuendeleza kazi hiyo.
Alisema ujenzi huo umefikia asilimia 98 ambapo kazi iliyosalia ni kuweka mfumo wa gesi ambapo fedha hiyo haitoshelezi kufikia asilimia 100 kwa makadirio ya ujenzi wa chumba kimoja ni Tsh,50.000,000.00 tofauti na Tsh,30,000,000 iliyopokelewa kwa ujenzi wa chumba kimoja.
Katibu tawala mkoani Songwe,Happinnes Seneda,alisema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imefanya kazi kubwa kuhakikisha kila kata uinakuwa na shule bora ya sekondari huku Rais akitafuta fedha kwa nguvu kuhakikisha shule zinajengwa hivyo hatarajii kuona wanafunzi wanapata alama sifuri.
Aidha Seneda,aliwaasa waalimu waongeze jitihada Zaidi kuhakikisha wanafunzi wanafauru mitihani kwa kupata alama A hadi C huku akisisitiza haitaji kuona alama D ama Sifuri ambapo pia aliwaasa wazazi kuharakisha suara la chakula mashuleni ili kumuongezea maarifa na uelewa mwanafunzi.
‘’Hawa ni Watoto wadogo wanahitaji kupata chakula shuleni ili kuondokana na udumavu,pia wakipata chakula wataongeza juhudi na kufanya vizuri darasani’’alisema Seneda.
Katibu huyo tawala yupo wilayani songwe katika ziaya yake ya kikazi ambapo ni muendelezo wa ziara hizo kwa mkoa mzima.
Comments