RAS SENEDA AGEUKA MBOGO KITUO CHA AFYA KUTOKUWA NA MPANGO MATUMIZI YA DAWA.
RAS SENEDA AGEUKA MBOGO KITUO CHA AFYA KUTOKUWA NA MPANGO MATUMIZI YA DAWA.
Na Rahimu Secha,Songwe
KATIBU tawala mkoani Songwe,Happines Seneda,amechukizwa na kitendo cha kutokuwepo kwa mpango mzuri wa upokeaji na utoaji wa dawa kwa wagonjwa katika kituo cha afya Ileza kata ya Magamga wilayani Songwe mkoani hapa.
Seneda aliyesema hayo juzi alipotembelea kituo hicho kujua hali ya uamilifu wa ujenzi majengo mapya pamoja na huduma za matibabu zilizoanza kutolewa ambapo alishikwa na butwaa kuona baadhi ya madudu hasa katika ukosefu wa taarifa za utoaji wa dawa kwa wagonjwa.
Kata ya Magamba iliyopo pembezoni mwa wilaya hiyo,ikiwa na zaidi ya wakazi 17.400 ambapo awali wananchi hao walikuwa wakitembea kulometa 18 kupata huduma za afya makao makuu ya wilaya yaliyopo kata ya Mkwajuni.
Sophia Mwashilindi,mkazi wa kijiji cha ileza alisema kituo hicho kimeanza kazi ya kutoa huduma na wao kuondokana na kadhia ya kutembea umbali huo wa zaidi ya kilometa 18 ambapo pia walilazimika kwenda kupata tiba a kienyeji kwa waganga wa jadi kutokana na ukosefu wa fedha za kusafiri umbai huo.
Alfonce Mponzi alisema wanaipongeza serikali ya Rais Samia kwa kuwapatia fedha kujenga kituo hicho ambapo kwa sasa kitapunguza wimbi la wananchi wakiwemo wajawazito kutibiwa nyumbani na kwa wakunga wa jadi mazingira yaliyopelekea vifo vya watoto wachanga na akina mama,na kwamba nyumba za watumishi pia zinatakiwa kujengwa.
‘’Katibu tawala tunakupongeza kwa jitihada za kuja hapa kujua maendeleo ya kituo hiki,hapa kuna tatizo la ukosefu wa dawa,pia daktari anayetegemewa anaishi kwenye kata nyingine ng’ambo ya mto,maji yakijaa hatakuwa na uwezo wa kuvuka hivyo endapo kutakuwa na wagonjwa hapa watakosa huduma wataweza kufa’’alisema.
Kaiza Mtafya mkazi wa Ileza alisema serikali imefanya kazi kubwa ya kuleta fedha kujenga kituo hicho,na wao wananchi wametoa nguvu kazi kuhakikisha ujenzi unakamilika na sasa baadhi ya huduma zimeanza kutolewa lakini kuna tatizo kubwa la ukosefu wa dawa,kila ukija unaandikishwa na kuambiwa kanunue dawa dukani hali hiyo imeleta usumbufu mkubwa.
Mganga mfawidhi wa kituo hicho,Timoth Simkonde alipotakiwa kujibu kuhusu shutuma hizo,hakuwa na majibu ya kuridhisha na kusema watajirekebisha na watakuwa wanatunza kumbukumbu ya dawa zinazoingia na kututumika.
Kaimu mganga mkuu wilayani humo,Dr Egfrid Mwingilihela, alisema ni kweli malalamiko hayo yapo na kuhusu mganga kukaa nje ya kata ni kutokana na ukosefu wa nyumba za watumishi hivyo jitihada za kujenga nyumba zinafanyika ambapo pia kuna mganga anayeishi katika eneo hilo ambaye ikitokea tatizo la mgonjwa muda wote anafanya kazti ya huduma,ambapo hadi sasa Tsh,Milioni 541,725,000.00 zimetumika kwenye mradi huo..
Aidha Dr,Mwingilihela,alizitaja changamoto zilizopo kwenye kituo hicho kuwa ni kutokamilika kwa majengo na kuchakaa kabla hayajafanya kazi kutokana na kukosa watoa huduma,ubovu wa miundombinu ya barabara,hali inayosababisha usafirishaji wa vifaa kuongezeka gharama pamoja na ukosefu wa maji.
Aliongeza kuwa utatuzi wa jambo hilo linaweza kutatuliwa katika bajeti ya 2013-2014 ambapo wanategemea kupata fedha za kukamilisha majengo yaliyosalia likiwemo la wagonjwa wa nje (OPD) kuhusu maji alisema wamewasiliana na Ruwasa ambao wameanza kushughurikia.
Hata hivyo aliishukuru serikali ya Rais Samia kwa kutoa vifaa kama Taa za upasuaji,Meza ya upasuaji,Jokofu la damu la benki ya damu,Mashine ya kufanyia uchunguzi na mkojo (Biochemia) ambapo ufungaji wa taa umefanywa na MSD kwa ktumia mafundi wao na kituo kimesajiliwa MSD na wameomba dawa na vitendanishi.
Katibu tawala mkoani humo kwa mara nyingne alitoa onyo kwa watumishi wa kituo hicho akiwataka waache uzembe wafanya kazi kwa kufuata taratibu za kiutumishi wakiendeleza uzembe watakiona cha mtema kuni huku akisisitiza upandaji wa miti 10 kila kaya kulinda mazingira kuhepuka majanga.
Mradi huo wa kituo hicho cha Ileza kipo kijiji na kata ya Magamba Tarafa ya Songwe ujenzi ulianza mwaka 2019 kwa utaratibu wa Force akaunti majengo yaliyopo ni jingo la wazazi, upasuaji ,Maabara,nyumba moja ya mtumishi,uendelezaji jengo la wagonjwa wa nje (OPD) lililokuwa likijengwa kwa mguvu za wananchi toka mwaka 2014.
Comments