SAZA-WILAYANI SONGWE WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAJENGEA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA TAA ZA BARABARANI



Na Rahim Secha,Songwe

WANANCHI wilayani Songwe mkoani hapa, wameipongeza Serikali kupitia wakala wa Barabara nchini (TANRODS) Mkoani Songwe kwa kuwajengea barabara sambamba na uwekaji wa taa eneo la Saza Hali iliyochochea kukua kwa uchumi.


Uwekaji wa taa hizo katika eneo la mzunguko (Round About) kumewezesha kata ya Sasa inayokuwa Kwa kasi kiuchumi kutokana na kuwa ni eneo la uchinbaji wa madini ya Dhahabu Hali inayovutia wawekezaji na wajasiliamali kuzidi kuwekeza zaidi.


Mussa Rashid dereva wa bajaji kutoka Mkwajuni kwenda Saza, alisema uwekaji wa taa hizo kunefungua mnyororo wa thamani kwani Kwa sasa wanalazimika kufanya kazi ya kubeba abiria hadi saa saba usiku ukilinganisha na awali ambapo walikuwa wakiishia saa moja hadi saa mbili usiku.


Albert Lusambo mchoma nyama na mkazi wa Sasa alisema anakila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu Kwa kuwajali wananchi wake na kwamba wanalazi mika kufanya biashara hadi saa nane usiku wakitumia mwanga wa taa hizo huku mji ukizidi kuchangamka.


Suma Mkalimoto mchoma mahindi na mkazi wa Saza alisema ujio wa taa hizo mji umechangamka na wao wamekuwa wakijiingizia kipato Kwa kufanya kazi hadi usiku wa manane hivyo anakila sababu ya kuipongeza Serikali kwa kutambua mahitaji muhimu ya wananchi.


Sarafina Issaka mama lishe na mkazi wa Songwe, alisema wamelazimika kufungua migahawa pembezoni mwa mradi huu kutokana na uwepo wa mwanga utokanao na taa hizo huku wajasiliamali wengi wakizidi kutafuta maeneo ya kufungua biashara na kuufanya mji wa Saza kukua kwa kasi kiuchumi..


Diwani wa kata ya Saza....... alisema kwa sasa anatembea kifua Mbele kutokana na Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suruhu kuiboresha barabara hiyo na kuweka taa ziilizofungua fursa za kiuchumi na kuupendezesha mji.


Alisema wakati ujenzi unaanza yeye pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya kata,Tarafa, Wilaya pamoja Mkoa walikuwa wakifika kuutembelea mradi huku wakipewa ushirikiano mzuri na mainjinia wa Tanroads hadi ulipo kamilika na kuleta tija za kiuchumi kwa jamii.


Mbunge wa Jimbo la Songwe Philipo Mulugo alisema katika kipindi hiki cha Rais Samia Miradi mingi mikubwa na midogo imekuwa ikijengwa kwa kasi na kuwashangaza wengi hadi wengine wakidiriki kusema wazi mama anaupiga mwingi na kwa kweli anaupiga hadi unafirumia.


Mulugo,, maarufu Kwa jina la Papaa mutu ya watu, alisema uwekaji wa taa hizo kumeufanya mji wa Saza kuwa kimbilio la wawekezaji na wajasiliamali na kwamba mbali na mradi huo,pia kuna miradi mikubwa ya liyotumia mabilioni ya fedha ambayo ni  Afya,Elimu,Maji, Miundombinu na Kilimo imeletwa huku fedha zaidi za miradi zinaendelea kuletwa.


Ifahamike kuwa wilaya ya Songwe ni Mpya iliyomegwa kutoka Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya miaka zaidi ya kumi iliyopita ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za ikosefu wa barabara Mzuri na za Lami,lakini kwa awamu hii barabara zimeboreshwa na  zinapitika ipo haja Serikali kuongeza tija kuharakisha ujenzi wa Barabara kuu ya kiwango cha Lami kutoka Mbalizi hadi Mkwajuni.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE