UJENZI WILAYAÑI SONGWE MATUNDU 15 YA VYOO SHULE YA MSINGI MWAMBANI
Na Rahimu Secha,Songwe
KUTOKANA na uwepo wa changamoto ya ukosefu wa matundu bora ya vyoo kwenye shule ya msingi Mwambani iliyopo wilayani Songwe mkoani hapa,hatimaye halmashauri ya wilaya hiyo imejenga matundu 15 yenye thamani ya Milioni 26,085.56. kwa ajili ya kunusuru wanafunzi na hadha ya kujisitili.
Hayo yalibainika leo wakati wa ziara ya kikazi iliyofanywa na katibu tawala mkoani humo akiwa na timu yake ya wataalam ambapo katika wilaya hiyo,ambapo akiwa katika shule hiyo aliweza kuyakagua matundu hayo ya vyoo na kuridhika na ujenzi.
Shule ya msingi Mwambani inawanafunzi 602 wavulana wakiwa 284 kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba,ambapo idadi ya matundu ya vyoo yaliyopo ni 12 kati ya hayo matundu 6 ni ya wavulana ambapo shule hiyo imepokea Tsh,Milioni 20,601 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 15 ambapo kati ya hayo matundu 7 ni ya wavulana.
Akizungumza leo (jana) kwenye ukaguzi huo,afisa elimu msingi wilayani humo,Michael Nzunda,alisema fedha ilipokelewa tarehe 15 Juni 2021 kiasi cha Tsh,Milioni 20.601,125.56 toka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa matundu 15 ya vyoo na hatimaye vyoo vimekamilika.
Alisema kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji na kata wameweza kujenga matundu ya vyoo kwa kutumia kiasi hicho cha fedha ambapo walipokea fedha kutoka (SAWASH) na kiasi cha Tsh,Milioni 5,484,000.00 ni nguvu za wananchi.
Katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda,alipongeza ujenzi huo na kusema kuwa kiklichobakia ni wazazi kuhakikisha wanawapeleka Watoto wao kupata haki zao za kimsingi za kupata elimu huku akisisitiza suala la chakula ili kumjenga vyema mwanafunzi kuelewa masomo.
Aidha Seneda akiongea na baadhi ya Wananchi aliowakuta maeneo hayo amewapa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba juu ya kila kaya kuhakikisha wanapanda miti kumi mipya hata kama ulishawahi kupanda siku za nyuma.Sambamba na hilo wamewataka Wananchi kuishi kwa amani kuepuka Vitendo ovyo kama vile mauaji na ujambazi.
Comments