JELA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 10

 Katika kesi hiyo ya jinai namba 69/2022,upande wa jamhuri umeweza kuthibitisha kosa hilo pasipo na shaka kupitia mashahidi wake wanne ikiwemo mtuhumiwa huyo kuthibitika kumlawiti mtoto huyo kwa nyakati tofauti kati ya Januari 2019 hadi Machi 13,2022.



Arusha. Mahakama ya Wilaya ya Arusha, imemhukumu kifungo cha maisha gerezani, Godlisten Kibwana (22), baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 10.



Kibwana ambaye ni mkazi wa eneo la Mianzini, jijini Arusha amehukumiwa adhabu hiyo leo Alhamisi, Desemba 29, 2022 na Hakimu Mkazi Bitony Mwakisu baada ya kumtia hatiani kwa kosa hilo la kumlawiti mtoto huyo kwa nyakati tofauti nyumbani kwao (mtuhumiwa).



Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mwakisu amesema mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo aliyekuwa anakabiliwa na kosa la ulawiti kinyume na kifungu cha 154(1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.


Amesema katika kesi hiyo ya jinai namba 69/2022, upande wa jamhuri umeweza kuthibitisha kosa hilo pasipo na shaka kupitia mashahidi wake wanne ikiwemo mtuhumiwa huyo kuthibitika kumlawiti mtoto huyo kwa nyakati tofauti kati ya Januari 2019 hadi Machi 13, 2022.



"Kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka ulionyesha mshtakiwa alikuwa na tabia ya kumwita mara kwa mara mhanga akiwa anacheza na wenzake na kumtuma  na anatumia fursa hiyo kumpeleka nyumbani kwao (kwa mshtakiwa) na kumuingilia kinyume na maumbile," amesema Hakimu


"Na hilo lilithibitishwa na mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani akiwemo daktari aliyemfanyia uchunguzi mhanga, mahakama imeridhika kesi dhidi ya mshtakiwa imethibitishwa bila kuacha shaka lolote hivyo mahakama imemtia hatiani mshtakiwa na kumpa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kuwa mhanga yuko chini ya miaka 18," amesema


Awali, Wakili wa serikali Upendo Shemkole aliomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwa wengine.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE