RC SONGWE AITAKA JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO YATIMA
Muhtasari
Jamii yatakiwa kuwakumbuka watoto yatimaa ,waishio katika Mazingira magumu na wajane hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba
Na Baraka Messa, Songwe.
JAMII Nchini yatakiwa kuwajali yatimaa, wajane na watoto waishio katika Mazingira magumu ili kutoa Faraja na kuwasaidia kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu ambayo wanayakosa.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Songwe Waziri Kindamba aliposhiriki chakula Cha pamoja na watoto yatimaa katika kituo Cha malezi ya kulea watoto yatimaa Mbozi Mission .
Alisema dini iliyo safi isiyo na takataka ni kuwajali watoto yatimaa, wajane na watoto waishio katika Mazingira magumu ambao hutaabika kwa kukosa mahitaji muhimu kutokana na kukosa wazazi, walezi na watu muhimu wa kuwasaidia na kuwajali.
" Kwa mujibu wa takwimu kutoka shirika la kimataifa la UNICEF jumla ya watoto milioni 140 Duniani kuanzia miaka 0 na kuendelea hawana wazazi Wala watu muhimu wa kuwaangalia,
pia kwa mujibu wa UNICEF Kuna takwimu za kusikitisha kila baada ya Sekunde 15 Duniani mtoto anapoteza wazazi kwa ugonjwa wa UKIMWI, hii Ina maana kuwa tuendelee kuwajali na kuwahudumia yatima" alieleza Mkuu wa mkoa.
Alisema Hata vitabu vitakatifu vya dini vinaeleza kuwafanyia mema wototo yatima , wajane na watoto waishio katika Mazingira magumu kwa kukosa Msaada kuwahudumia katika Jamii.
Awali akisoma taarifa ya kituo hicho cha Mganga Mkuu mfawidhi wa Hospital ya Mbozi Mission Asel Pwele alisema kituo hicho kilianzishwa ya mwaka 1940 na kukamilika 1949 ambapo kilianza kufanya Kazi chini ya kanisa la Moravian.
Alisema kituo hicho kina uwezo wa kulea watoto wapatao 12 kwa wakati mmoja na kwamba hivi sasa kina watoto 7 watoto wapatao wenye umri wa kuanzia siku moja hadi miaka 23.
Alisema watoto hao wanapata haki zote ambazo mtoto anatakiwa kupata , ambapo Msaada mkubwa inatoka kwa wadau mbalimbali wanaoguswa ndani ya mkoa wa Songwe na nje ya mkoa .
Mkuu wa kituo hicho Cha kulelea watoto yatimaa katika kituo hicho Cha hospital ya Mbozi Mission Anes Wavenza alisema kati ya watoto 7 wa waliopo kituoni hapo watoto wanne wana umri chini ya miaka Saba ambapo huhitaji huduma za ukaribu zaidi.
"Kati ya watoto wanne wenye chini ya umri wa miaka Saba, Watoto wawili ambao ni mapacha waliletwa Hapa wakiwa wachanga baada ya mama yao kufariki wakati wa kujifungua, mtoto mwingine aliletwa baada ya mama yake kujifungulia njiani na kupoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi , Lakini mtoto wa mwingine ambaye ni Mlemavu wa ngozi aliletwa kwa ajili ya usalama zaidi kutokana na Jamii kuwa na Imani za kushirikina " alisema Anes.
Comments