RC SONGWE APOKEA MADARASA KIMKOA TUNDUMA,ASIFU UJENZI WA MADARASA NDANI YA MKOA WA SONGWE
Na Raheem SECHA,Tunduma
Mkuu wa Mkoa kwa Songwe Mhe. Waziri Waziri Kindamba leo Disemba 31, 2021 amepokea madarasa katika Wilaya ya Momba kwa niaba ya Mkoa wa Songwe
Akiongea katika Hafla hiyo Mhe. Kindamba amesema ameridhishwa sana na ujenzi wa madarasa ndani ya mkoa wake na hususani hapa Halmashauri ya Mji Tunduma alipokuja kufanya uzinduzi ya kuyapokea madarasa kimkoa
“Nawapongeza sana Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kweli mmeitendea haki Pochi ya mama Samia, Nimeridhika sana na ujenzi wa madarasa yote 12 tena ninyi mmejiongeza zaidi mmejenga na ofisi hongereni sana” alisisitiza Mhe. Kindamba
Wakati akikagua vyumba vya madarasa hayo 12 Mhe. Kindamba ameeleza kuwa Madarasa yana Malumalu, madirisha ya Aluminum, Dari za kisasa (Gypsum board), miundombinu ya Umeme, na Madawati 50 kila darasa ni hatua nzuri sana na ndio maana anayaita ni madarasa ya kimataifa
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Songwe amewaalika wazazi kuwa ifikapo Januari 09, 2023 wanafunzi wote wanatakiwa kuanza masomo hivyo kila mzazi ahakikishe kuwa mwanafunzi anaripoti shule bila kikwazo
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayongozwa na Rais Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha na kujenga madarasa pamoja ununuzi wa madawati bila kusahau vifaa vya kufundishia na kijufunzia hivyo hatuna upungufu wa kitu chochote ndani ya Mkoa wa Songwe kinachoweza kusababisha wanafunzi wasianze masomo, ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto wake anaanza masomo mara moja” alisisitiza Mhe. Kindamba
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Fack Lulandala alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuwa Wilaya ya Momba ina Halmashauri Mbili yaani Halmashauri ya Wilaya ya Momba na Halmashauri ya Mji Tunduma ambapo Momba ilikuwa na ujenzi wa Madarasa 16 na Tunduma ilikuwa na ujenzi wa Madarasa 12, madarasa yote 28 yamekamilika na Wilaya ya Momba haina upungufu wa Madarasa kwa sasa
“Momba tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za ujenzi wa madarasa kwa ajili ya kidato cha kwanza na tumetekeleza kwa kiwango cha kimataifa. Tunamumbea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia Afya njema ili azidi KUUPIGA MWINGI” Alisema Mhe. Lulandala
Pia Mhe. Lulandala amekemea wazazi wanao waficha Watoto kuanza shule kwa sababu zozote zile waache kwani sheria itauchukua mkondo wake
“Rai yangu kwa wazazi wanaokwamisha Watoto kuanza masomo kwa sababu ya kuwaachia Watoto majumbani au kuwatumikisha kwa namna yoyote ile nasema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mzazi yoyote yule bila kujali wadhifa au cheo alichonacho” alisema Mhe. Lulandala
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Bi. Patricia Mbigili amesema kuwa Halmashauri ya Mji Tunduma sasa inakua kwa kasi kutokana na kuwepo kwa shule nzuri zinazoendela kujengwa
“Madarasa haya 12 tunayokabidhi leo yatasaidia wanafunzi ambao wameongezeka kwa asilimia kubwa kutokana na kuwepo kwa elimu Bure, pia kutonaka na Ubora na uzuri wa madarasa wanafunzi wengi tunategemea wataacha utoro kwani mazingira haya ni mazuri kwa kujufunza na kufundishia. Hivyo Ubora wa elimu hasa kwa Tunduma Mji utapanda zaidi” alisisitiza Bi. Patricia
Comments