AFISA TARAFA MBOZI AGAWA MICHE 1000 YA MITI IKAPANDWE KWENYE KAYA KAMA AGIZO LA MKUU WA MKOA LINAVYOTAKA UPANDAJI MITI


Zoezi la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe Omary Kindamba la kupanda miti kila kaya ndani ya Mkoa wa Songwe likiendelea kutekelezwa maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Songwe. Wilaya ya Mbozi kupitia afisa Mazingira Hamis Nzunda wameanza kutekeleza kampeni hiyo kwa Tarafa za Wilaya ya Mbozi na zoezi hilo linaendelea kwenye Tarafa ya Iyula 


Edward Lugongo afisa tarafa ya Iyula amezindua kampeni ya upandaji miti katika kata ya Ruanda iliopo Tarafa ya Iyula ambapo zaidi ya Miti 1000 imetolewa Kwa kaya mbali mbali katani hapo ambapo kila kaya imepata miti mitano na mingine mitano kila kaya itajighalamia yenyewe Ili kufikia kumi kama agizo la Mkuu wa Mkoa linavyotaka Kila kaya kupanda miti kumi.

"Tunawapeni miti hii mitano mitano kama kuwahamisha lakini Kila kaya inatakiwa kupanda miti kumi na ni jukumu letu kuitunza miti hii na ifikapo tarehe 15 ya mwezi huu tutaanza kukagua kama kila kaya imepanda miti na atakae kaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria na faini zitamuhusu" alisema Lugongo kabla ya kukabidhi miti hiyo.




Aidha Lugongo amewataka Viongozi wa kata wakiwemo Viongozi wa Vijiji kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo la upandaji miti na kutaka kumchukulia hatua yoyote atakae vuruga zoezi hilo.

Kwa upande wake afisa mazingira Wilaya ya Mbozi Hamisi Nzunda amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na watafanya kata zote hivyo amewasihi Wananchi wa Mbozi kuhakikisha wanaitunza miti hiyo na kutoa onyo kali kwa wenye tabia za kuchungia mifugo jirani na miti itakayopandwa hatua kali zitachukuliwa bila kumuonea haya mtu.

Maria Babuya Mkazi wa Ruanda ameishukuru Serikali kwa kuwapa miti hiyo mitano bure na kuahidi kuitunza na  ameongeza kuwa watakwenda kununua mingine mitano Ili ifika kumi

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE