BEI ZA VOCHA ZA SIMU ZAPAA MJI WA MLOWO,MKOA SONGWE

Bei za vocha za mitandaa mbalimbali ya simu za mikononi zimepaa katika Mji wa Mlowo uliopo katika Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe sababu kuu ikiwa wauzaji wa jumla wamepandisha bei ya kujumlia vocha hizo.


Katika maduka mengi ya Mji wa Mlowo vocha zimepanda ambapo vocha shilingi 500 inauzawa shilingi 600 na vocha shilingi 1000 inauzwa kati ya 1100 hadi 1200 kutokana na bei atakayokutajia muuzaji.


Mwandishi wetu alishuhudia mteja wa vocha akiuziwa vocha ya mtandao mmoja Kwa shilingi 1200 na mnunuzi alipopuliza sababu alijibiwa kuwa wauzaji wakubwa wa vocha Mlowo wamepandisha bei za Vocha za Jumla.


"Kiukweli Mji wa Mlowo inabidi Serikali itusaidie kuna wajanja wengi wanapandisha vitu watakavyo wao Mbolea wamejipandishia bei sasa Hadi vocha jamani tamaa hizi mbona zimezidi zamani walisingizia mafuta yamepanda bei sasa sijui watasingizia nini"alilalamika Suzana Mwamengo Mkazi wa Mlowo kwa Maswala.


hata hivyo kuwatafuta wafanyabiashara wakubwa wa kujumlisha vocha Mlowo lakini asilimia kubwa tuliwakuta wafanyakazi wao maofisini na walidai waulizwe mabosi wao.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE