TFS,MARMO WAING'ARISHA MBOZI AGIZO LA RC LA UPANDAJI MITI LAANZA KUTEKELEZWA KWA KASI

.       (Afisa Mazingira Wilaya ya Mbozi Hamisi Nzunda)
 

Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe la Upandaji miti Mkoani Songwe linaonekana  kutekelezwa kwa vitendo na kasi kubwa Wilayani Mbozi ambapo karibu kila tarafa zinaendelea na zinduzi  mbalimbali za upandaji miti.


Afisa mazingira Wilaya Mbozi Hamisi Nzunda amesema wao kama halmashauri wamelipokea agizo  la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba na wameanza pia kuwashirikisha wadau mbalimbali ambapo tayari wamepata baadhi ya miche na wameanza kuigawa kwa kaya miche mitano na mingine mitano wanakaya watajinunulia

      (Meneja Tfs Mbozi Fred Mgeni)

"hili naomba niliweke sawa tuna baadhi ya wadau wamejitolea kutupa miche na sisi tunaigawa kwa Wananchi ni miche michache hivyo haiwezi kuwatosha wote hivyo niseme tu neno kwa Wananchi kuendelea kutafuta miche na kupanda kwani hatua ya ukaguzi kila kaya utafuata"-amesema Nzunda


Aidha Nzunda amewashukuru wadau mbalimbali wanaojitolea miti ya kupanda katika kipindi hiki cha kampeni ya upandaji miti amewashukuru sana TFS  lakini pi amewashukuru kampuni ya uchimbaji madini ya malumalu ya MARMO ilijitolea miti 260 hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza na kujitolea miti 


Kwa upande  wake meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Fred Mgeni  amewataka wakazi wa Wilaya Mbozi kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi na kuitunza kwani Wilaya ya Mbozi ni moja ya Wilaya zinazoongoza kwa ukataji miti kwa wingi na uchomaji mikaa na wamekuwa wakiwakamata wanaofanya uharibufu huo na kuwachukulia hatua hivyo sasa Wananchi watambue umuhimu wa kupanda miti kwa ustawi wa Taifa la Tanzania na pia kutunza mazingira yao binafsi.


Aidha kwa upande wa wao kama Wakala wa huduma za misitu wametoa na wanaendelea kutoa miche katika kipindi hiki cha kampeni ya upandaji miti kimkoa hivyo watakuwa bega Kwa bega na halmashauri ya Mbozi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE