BREAKING NEWS: RC SONGWE AMSIMAMISHA MWENYEKITI MAGESA AVIKABIDHI VYOMBO VIMCHUNGUZE
Kufuatia sakata la Mwenyekiti wa watumia Maji Mji wa Mlowo Poul Magesa kulalamikiwa na wananchi kufanya vitendo visivyoendana na Maadili ya kazi ikiwemo kuchukua kuwapiga watu faini na kutowapa risti Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba amemsimamisha Mwenyekiti huyo sambamba na kuviagiza Vyombo ya usalama Mkoa wa Songwe shutuma zinazomkabili na ikibainika hatua kali zichukuliwe dhidi yake
Kindamba amesema amesikia malalamiko ya Wananchi na Serikali ya awamu ya sita ipo Kwa ajili ya kusikiliza Wananchi hivyo kitendo kinacholalamikiwa na Wananchi hakiwezi kuachwa hivyi hivyo ni lazima kichunguzwe na ikibainika hatua zaidi zitachukuliwa
"Kwa sasa namsimamisha na kuviagiza Vyombo vya usalama kuchunguza shutma zake na ikibainika apelekwe vyombo vya sheria Ili sheria ichukue mkondo wake.
Aidha Wananchi wa Vijiji vya Mbozi na Msuto wamejitokeza na kutoa malalamiko mapya kuwa aliwaamulu kufyeka mazao yao ya mahindi na kuwapiga faini ya laki tatu na walipoomba risti aligoma kuwapa
Comments