MBOZI WAZIDI KUJIIMARISHA KIMAZINGIRA WAZINDUA UPANDAJI MITI KATA YA NANYALA
Diwani wa kata ya Nanyala ambae pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbozi George Mushani amezindua rasmi kampeni ya upandaji wa miti katika Tarafa ya Iyula ambapo Uzinduzi huo umefanyika katika kata ya Nanyala.
Kabla ya kuzindua kampeni hiyo Mushani waliwaeleza Wananchi waliofika katika Ofisi za kata ya Nanyala kuwa kampeni hiyo si kwa ajili ya Serikali tu bali ni faida kwa Wananchi na ustawi wa nchi ndio maana miti hiyo wanawapa wakapande kwenye kaya zao na ni jukumu la kila Mwananchi kuitunza miti hiyo.
"Niwaombe sana Wananchi tuitunze miti hii mpaka ikue ili utusaidie sisi na vizazi vyetu vijavyo"
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Mushani amaechangia kiasi cha shilingi laki mbili ili zitumike kununua miche mingine na nikatika kufunga mkono juhudi za agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba kupanda miti kumi Kila kaya vijijini na Miti mitano kaya za mjini.
Katika Uzinduzi huo pia ukihudhuliwa na afisa tarafa ya Iyula Edward Lugongo ambae ameendelea kuwasisitiza watendaji wa Serikali na Wenyeviti wa Vijiji kuhakikisha zoezi hilo wanalisimamia na wasisite kumchukulia hatua yoyote atakaejaribu kuharibu zoezi hilo na kuwakumbusha Wananchi kuwa kutakuwa na zoezi la ukaguzi wa miti hiyo kila kaya na asietekeleza hatua kali zitafuta dhidi yake.
Uzinduzi huo pia pia ulihudhuliwa na afisa mazingira Wilaya Hamisi Nzunda,meneja tfs na Viongozi wengine kazi ya kata na wilaya
Comments