MENEJA LATRA SONGWE AFANYA UKAGUZI WA NAULI NA TIKETI STENDI VWAWA
"Nimekuja hapa mwenyewe baada ya kupigia simu na abiria kuwa amekatiwa shilingi 700 na daladala toka Hanseketwa mpaka Vwawa badala ya shilingi 500 tumeikamata Daladala na abiria amerudishiwa cheji yake na tumeipiga faini daladala hiyo"amesema meneja
Katika hatua nyingine Latra imefanya ukaguzi kwenye mabasi yaendayo Mkoa jirani wa Rukwa ambapo katika ukaguzi wa baadhi ya mabasi yamekutwa hayajatumia tiketi za mfumo wa kieletroniki na baadhi zikiwa zimeandikwa kwa mikono.
( Meneja akiwaelekeza makondakta jinsi ya kutumia simu janja Ili kujua bei halisi za nauli Mikoani)Sambamba na hayo Meneja wa latra alitoa elimu kwa makondakta kutumia simu janja Ili kujua viwango halisi vya nauli na kuacha tabia ya kujiongezea nauli kiholela. Pia Meneja ametoa rai kwa wamiliki wa daladala Mlowa,Vwawa mpaka Tunduma kuhakikisha wanaandika bei za nauli jirani na milango ya daladala zao kabla hatua dhidi yao hazijaanza kuchukuliwa
Comments