RC SONGWE " TUTASHIRIKIANA NA VIONGOZI WA KIMILA KUKUZA VITUO VYA UTALII WA MKOA WA SONGWE ILI TUWEZE KUKUZA PIA UCHUMI KUPITIA UTALII"


Mkuu wa mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amesema mkoa huo umejipanga kuvumbua vivutio vya kitalii ili kuimarisha uchumi kupitia sekta ya utalii.


Kindamba amesema hayo leo Jumatano Desemba 4, 2023 wakati alipoambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kutembelea baadhi ya maaeneo ya vivutio vya kitalii yaliyopo katika mkoa huo.


Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa mkoa pia  ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe (RAS), Happiness Seneda na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi George Musyani.

Wengine walishiriki katika ziara hiyo ni viongozi wa dini  akiwemo Shekhe Hilal Kipozeo na Mchungaji maarufu Richard Hananja na baadhi ya machifu.


Miongoni mwa maeneo ambayo viongozi hao walitembelea ni pamoja na michoro na unyayo ya kale Nkangamo wilayani Momba, majimoto kata ya Nanyala na kimondo cha Ndolezi Kata ya Mlangali vyote vilivyopo wilaya ya Mbozi.


Ziara hiyo ni utekelezaji wa mikakati ya mkoa huo ya kuboresha maeneo ya vivutio vya utalii na  kutunza misitu na vyanzo vya maji ili kuvutia watalii na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika ziara hiyo, Kindamba amesema kuwa "Tunaibua vivutio vya kiutalii na kujua tulipotoka tujue tunapotoka kwenda. Tumekuja kujifunza na kuviibua"  


"Tunataka kujenga uchumi kupitia sekta ya utalii" amesema mkuu huyo wa mkoa


Ametaja mambo ambayo yataweza kusaidia mkoa huo kufungua uchumi kupitia utalii kuwa ni pamoja na; Kuboresha moundombinu, kuweka mikakati ya uchumi na kuibua vivutio hivyo na kuvitangaza.


Kindamba amesema kuwa wametembelea maeneo hayo kujifunza ili kuangalia namna ya kulifanya eneo hilo liwe la kiuchumi.


"Tumekuja kwenye eneo la utalii tujifunze tuone eneo hili kulifanya liwe la kiuchumi Ili kuingiza fedha


Tumeona changamoto hasa barabara tutaongea na watu wa Tarura ili tuweze kutengeneza moundombinu ikae vizuri" amedokeza


Amebainisha kuwa lengo la kutembelea vivutio hivyo ni kuvitangaza ili dunia ivijue.


"Tumetembelea vivutio ili kuviibua na kuvitangaza ili dunia na Tanzania wajue Songwe tuna aina gani ya vivutio. Japo kwa uchache watu wavione maana kwa ujio wao fursa za kiuchumi zitafunguka"


Naye Abraham Siame ambaye ni chifu msaidizi amesema "wazazi wetu walitueleza michoro waliikuta hawajui ni mwaka gani ilichorwa nao wanasimuliwa na mababu zao wa zamani"


Kwa upande wake msimamizi mhifadhi kimondo Mbozi, Andru Lowasa  amesema kuwa katika eneo hilo wamepata mabaki ya zamani yakiwemo vyungu vya zamani.


"Tulichimba tulifanikiwa kupata vyungu vya zamani, ilikua inaishi kwenye jamii za kiwindaji, na michoro hii ilichorwa na utomvu wa miti" amesema


Mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikoa yenye vivutio vingi vya utalii vikiwamo; Kimondo kinachopatikana Ndolezi wilayani Mbozi, maporomoko ya maji moto, michoro ya zamani, maeneo ya historia ya machifu wa zamani ikiwamo sehemu ambayo hufanyika matambiko ya kimila.


Pia mkoa huo ni miongoni mwa mikoa maarufu kwa uzalishaji wa chakula nchini ambapo huzalisha mazao mablimbali ikiwemo mahindi, mpunga, kahawa, viazi na parachichi.


Mkoa huo umeanza jitihada za kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri nchi na dunia.


Miongoni mwa mipango iliyoanzisha na mkoa huo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na kampeni maalumu ya kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.


Katika kampeni hiyo maalumu ya upandaji miti ili kutunza mazingira, kila kaya maeneo ya mjini inatakiwa kupanda miti mitano na kaya za vijijini miti 10.


Pia, taasisi au kampuni zinatakiwa zipande miti kulingana na ukubwa wa maeneo yao huku kila kitongoji kikitakiwa kuwa na siku maalumu ya kupanda miti ambapo wenyeviti wa vitongoji watasimamia siku hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE