SONGWE WATUMIA MAZOEZI KUHAMASISHA UANDIKISHAJI WANAFUNZI SHULEN
Viongozi wa Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na wananchi, Taasisi binafsi na za Serikali wametumia mazoezi ya jogging kuhamasisha uandikishaji wa wanafunzi shuleni haswa kwa kidato cha kwanza ambao hadi sasa ni 76 ndio waliofanikiwa kuripoti shuleni.
Mazoezi maalumu ya jogging ambayo yameitwa kwa jina la Back to School special jogging yenye lengo la kuhamasisha wanafunzi kujiandikisha shuleni yamefanyika leo, 21 Januari kwa Wilaya zote za Mkoa wa Songwe na kimkoa imefanyika wilayani Mbozi na kuongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi.Happiness Seneda amewataka wazazi kuendelea kuwapeleka watoto shuleni hususani kidato cha kwanza ambao idadi kubwa ya wanafunzi bado hawajaripoti shule ikiwa mpaka sasa ni asilimia 76% ndio waliofanikiwa kuripoti, uku darasa la awali ni 82%, la kwanza ni 96%.
"Tunataka watoto wote wafike shuleni ata kama hana sare, daftari au mahitaji yoyote ya Shule kwani Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tuweze kujua wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili tuweze kuona namna ya kuwasaidia" Bi. Happiness Seneda.
Katibu Tawala, Bi. Happiness Seneda amesema kidato cha kwanza bado uhamasishaji kwa wazazi/walezi unahitajika kwani kwani kuna baadhi ya wazazi wanawatumia watoto kwenye Kilimo ukizingatia saizi ndio msimu wa Kilimo jambo ambalo ni kosa kisheria kuwatumia watoto shambani muda wa masomo.
Afisa Elimu Mkoa wa Songwe, Mwl. Michael Ligola amesema hadi sasa shule zipo wazi siku zote wanafunzi wanapokelewa mashuleni hivyo kila mzazi ampeleke mtoto shuleni.
Katibu wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe, Ndg. Juma Mpeli ametoa wito kwa kila mwananchi, Taasisi zote kwa kushirikiana na Serikali kwenda kuhamasisha watoto waende Shule.
Serikali ya awamu ya sita imejitahidi chini ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha miundombinu ya Shule kwani hadi sasa hakuna matatizo ya madarasa ila kuna tatizo la wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni ila madarasa na madawati vinawasubiria wanafunzi tu, ameeleza, Ndg. Juma Mpeli Katibu wa CCM Mkoa.
Comments