TABIA ZA WABUNGE MKOA WA SONGWE ZAMKERA MWENYEKITI CCM MKOA

 


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe Radwell Mwampashe ameshangazwa na baadhi ya Wabunge Mkoani Songwe kutofika ofisi za Chama kujitambulisha kwa  Uongozi wa chama ambao uchanguzi wa Viongozi hao ulifanyika mwishoni mwa mwaka 2022.Akiongea atika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wilaya wapya Wilaya  za Mkoa wa Songwe waliopata uteuzi wa Rais hivi Karibuni hafla iliofanyika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe makao makuu ya Mkoa Mbozi.


Radwell amesema Wabunge wa Mkoa wa Songwe baadhi hawajui sababu hawajafika katika Ofisi yake kujitambulisha na amemueleza Mhe Mlugo kama Mwenyekiti wao kuwafikishia salamu zake Wabunge hao kwani itafika kipindi  chama kitashindwa kuwasaidia pindi wanapopata changamoto.


"Mhe Mlugo wewe huwa nakuona na umefika ofisi za Chama wengine nawashangaa hawataki kuja kujitambulisha na kufika ofisini kwangu waambie utafika muda wao wa kututafuta maofisini"alisema Mwenyekiti Radwell


Aidha upande wa Wananchi baadhi ya Wanachama wa CCM waliokuwepo ndani ya hafla hiyo kwa nyakati tofauti wameunga mkono taarifa ya Mwenyekiti wao na kuwashutumu baadhi ya Wabunge wa kuwa hawaonekani hata kwenye shughuli za kijamii na haieleweki huwa wanashinda wapi lakini pindi wakisikia baadhi ya Viongozi wa kitaifa wanakuja Songwe nao hujisogeza jirani na Chama na Wananchi Ili waonekane kuwa wana mahusiano mema na chama kumbe ni maigizo tu hivyo wametaka kauli ya Mwenyekiti wa Chama waichukulie kwa uzito na kama njia ya wao kujikosoa.


Victor Mwaliego aliejitambulisha kuwa kada wa CCM  amesema Wabunge wa Songwe ni tofauti sana na Wabunge wa Mikoa mingine hawa wetu wazito sana sasa kama chamani tu hawapaheshimu Wananchi watawaheshimu kweli? Alihoji Mwaliego

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE