ULAWITI,UBAKAJI NA MAUAJI KAMANDA SONGWE AWATUMA SALAMU KUPITIA JOGGING"JESHI LA POLISI TUMEJIPANGA"
Mamia ya Wananchi wa Mkoa Songwe wamejitokeza katika mazoezi ya pamoja Jogging iliofanyika Wilayani Mbozi mapema leo asubuhi katika Viwanja vya CCM Mbozi.kabla ya kuingia katika Viwanja hivyo kulitanguliwa na mbio fupi zilizoanzia boma la Halmashauri ya Mbozi mpaka Ilembo eneo maarufu kama Mtambwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Theopista Malya akiongea na mamia ya Wananchi wa Songwe waliojitokeza katika Jogging hiyo wakati wa salamu za Viongozi amekemea tabia ya mauaji husasani Wilaya ya Mbozi ambapo amesema jeshi la Polisi limejipanga vilivyo kuhakikisha linakomesha tabia hiyo ambapo pia amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo pindi wanapopata taarifa au kumuhisi mtu anajiuhusisha na tabia za kihalifu na pia kamanda amewasihi Wananchi pindi wanataka kurudi nyumbani usiku wawatumie bodaboda au bajaji wanaowafahamu vyema Ili kuepuka kufanyiwa vitendo vya kiharifu na hata kuuwawa ambapo kamanda ametolea mfano mauaji ya mfanyakazi wa Tanesco Songwe ambae inadaiwa aliuwawa na dereva wa bajaji wakati alimrudisha Nyumbani kwake usiku.
Katika matukio mengine kamanda ACP Mally amesema kumekuwepo na Vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa Watoto wa shule za Sekondari na Msingi ambapo jeshi la Polisi limepokea kesi nyingi.
"Ndugu zangu Watoto wetu wameharibiwa vibaya mno Wazazi wachunguzeni Watoto wenu kesi nyingi tunapata za vitendo vya ubakaji na ulawiti tukiwachunguza watoto wetu na wataalamu wa afya wengi wameharibiwa sana sehemu zao za siri sisi kama jeshi tunaonya wenye vitendo hivyo na hatutosita kumchukulia mtu hatua kali zitachukuliwa"amesema kamanda.
Comments