UZINDUZI SIKU YA WIKI YA SHERIA NCHINI KANDA YA SUMBAWANGA
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Rukwa wameiomba Wizara ya Katiba na Sheria, kupitia upya sheria iliyoanzisha mabaraza ya kata nchini, ili yafanye kazi kwa mujibu wa sheria, tofauti na ilivyo hivi sasa mabaraza hayo ya kata yamekuwa yakitoa hukumu kwa wananchi badala ya kufanya usuluhishi.
Wakazi hao wameyatoa maombi hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria Mjini Sumbawanga, Mkoani Rukwa, kwamba utendaji wa mabaraza hayo kwa kutokufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi, migogoro ya ardhi imekuwa haiwezi kwisha katika maeneo mengi ya nchi.
Wamesema ikiwezekana mabaraza hayo ya kata yafutwe, kwakuwa yamechangia kwa kiasi kikubwa kutengeneza migogoro miongoni mwa jamii, kwa kuwa tu wanafanya kazi ambazo sio za kwao.
Msimamizi wa Baraza la ardhi la wilaya ya Sumbawanga, JUSTINA RWEZAURA, amekiri kweli mabaraza ya kata yamekuwa yakitoa hukumu ya mashauri yanayowafikia huko Vijijini, wakati sheria haijawapa mamlaka ya kutoa hukumu wanaposikiliza mashauri ya ardhi, badala yake mabaraza ya ardhi yamepewa mamlaka ya kusuluhisha pekee
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga SEBASTIANI WARYUBA ambaye amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa wiki ya sheria Kanda ya Sumbawanga, amesema wananchi waachane na utamaduni wa kupenda kesi na kuwa sehemu ya kusababisha migogoro ya ardhi ambayo haiwezi kwisha katika jamii.
Amewaomba watumishi wa Makama kuu ya Tanzania, kufanya kazi kwa weledi, na kuachana na vitendo vya kudai na kupokea rushwa, vitendo hivyo vimekuwa vikiifedhehesha mahakama nchini, na wananchi kutoa tafsiri kuwa mahakama inapindisha haki katika eneo ambao ndio watoa haki.
Aidha Jaji Mfawidhi Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga Dunstan Ndunguru amesema kauli mbiu ya Mwaka huu inayosema ‘’Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya Usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu,wajibu wa mahakama na wadau na kuwa kauli mbiu hii imebeba tafakari kubwa kwa mahakata katika utatuzi wa migogoro kwa jamii kwa usuluhishi hupunguza gharama za mashauri na kufanya wananchi kushiriki shughuli za uchumi na sio kutumia mda mwingi mahakamani.
Pia kwa upande wake mwakilishi wa mawakili wa kujitegemea Mkoa wa Rukwa Peter Kamyalile amesema wanapenda kesi kuisha mapema japo uwepo wa mawakili wasiopenda kesi kuisha mapema kwa ajili ya maslahi yao huku Musa Gyvnah kutoka Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa(TAKUKURU) akisema wameweka mkakatai bora wa kushirikiana na wadau katika kukomesha vitendo vya Rushwa.
Comments