WATUMIA MAJI MLOWO WAMTOSA RASMI MAGESA,WACHAGUA VIONGOZI WAPYA


 Kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba kutaka mamlaka zinazomsimamia Mwenyekiti wa jumuia wa watumi Maji Mlowo Poul Magesa kumsimamisha na kuviagiza Vyombo vimchunguze kutoka na malalamiko ya kutumia ubabe na lugha zisizofaa kwa Wananchi pia matumizi mabaya ya madaraka.


Leo katika Ukumbi wa shule ya sekondari Mahenje umefanyika uchaguzi wa Jumuiya hiyo na kupata Viongozi wapya huku Jumuiya hiyo ikiagana na Magesa rasmi na kumaliza historia yake ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo huku akisubiria majibu ya uchunguzi dhidi yake unaofanywa na Vyombo vya dola na endapo itabainika basi safari ya kupelekwa mahakamani kwake haitokwepeka.

 Katika hali ya kushangaza Mbunge wa Jimbo la Mbozi George Mwenisongole aliibuka katika Mkutano huo na kusema ameshangazwa na uwepo wa uchaguzi huo na yeye kutokupewa taarifa na amesema Mkuu wa Wilaya ya Mbozi na Ocd wa Mbozi wanapaswa kuwajibishwa kutokana na kile kinachodaiwa kumkumbatia na kumtetea Magesa ikiwa ni pamoja na kukalia kimya malalamiko ya Wananchi pindi wanapolalamika na kushindwa kuchukua hatua

Hawa ndio Viongozi wapya wa Jumuiya ya watumia maji-Mlowo


Dominick Mwamwezi ( Mwenyekiti)


Krosi Nzunda ( Makamu Mwenyekiti


Itika Mtawa ( Muhasibu)


Esnath Kalonge



Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE