BILIONI 4 ZAPELEKWA MBOZI KUJENGA BARABARA KUPITIA TARURA: SILINDE
Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Bajeti ya wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) katika Halmashauri ya wilaya ya Mbozi imeongezeka mara nne hadi kufikia shilingi bilioni 4 katika mwaka wa fedha 2022/23.
Amesema hayo leo tarehe 14 Februri 2023 wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mlowo katikaHalmashauri ya wilaya Mbozi mkoani Songwe.
“Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani alikuta bajeti ya TARURA katika Halmashauri ya Mbozi ilikuwa bilioni 1.7 lakini kwa sasa bajeti imepanga kufikia bilini 4 katika mwaka wa fedha 2022/23” amesema Mhe. Silinde
Amesema kupitia mradi wa kujenga barabara katika maeneo ya uzalishaji wa mazao ya kilimo “Agri-connect”, barabara ya Ilolo - Ndolezi yenye kilometa 11 inajengwa kwa Kiwango cha lamikatika katika wilaya ya Mbozi ambayo inaanza kutekelezwa hivi karibuni.
Aidha, Mhe. Silinde amesema katika awamu ya pili ya Mradi wa Agri-connect, barabara kutoka Mlowo mpaka Isanza ya kilometa 10 itajengwa kwa Kiwango cha lamiili kuwezesha wakulima kusafirisha mazao yao.
Katika Sekta ya Elimu, Amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta bilioni 1.32 kwa ajili ya kujenga madarasa katika Halmashauri ya Mbozi ili kuwezesha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaingia darasani kwa wakati Mmoja.
Mhe. Silinde amesema Shule Maalum ya sayansi ya Wasichana ya Mkoa wa Songwe ya shilingi bilioni 4 inaendelea kujengwa katika mkoa wa Songwe ambayo itapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Kadhalika, Silinde amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameboresha utoaji wa huduma za afya kwa kuwezesha ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Mbozi ambayo imeanza kutoa uduma za awali.
Pia. Mhe. Silinde amesema Ujenzi wa vituo vya afya vipya sita unaendelea katika Halmashauri ya Mbozi ambapo jimbo la Vwawa vinajengwa vituo vya afya vitatu na jimbo la Mbozi vinajengwa vituo vya afya vitatu.
Comments