DC MBOZI AKABIDHI PIKIPIKI KWA WATENDAJI KATA 9 ZA MBOZI,DED NANDONDE ATAKA WAZITUNZE


Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC), Esther Mahawe amekabidhi pikipiki tisa kwa watendaji wa kata ambazo zitawasaidia katika kutekeleza majukumu yao.


Mkuu wa wilaya huyo  amekabidhi pikipiki hizo leo Ijumaa Februari 17, 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.


Akikabidhi pikipiki hizo, mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa usafiri huo utawarahisishia watendaji hao wa kata hizo za pembezoni kutimiza majukumu yao kwa wakati.


DC Mahawe ametumia nafasi hiyo kuwaagiza watendaji hao kwenda kuwafuatilia watoto ambao bado hawajaripoti shuleni ili waweze kujiunga na wenzao kuendelea na masomo


"Naomba sana tuungane kwa pamoja tumsaidie mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) juhudi kubwa anazofanya katika kuwasaidia wananchi wake" ameagiza DC huyo.


Amekumbusha watendaji hao kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo vya moto Ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (DED) Abdallah Nandonde amezitaja kata zilizopata pikipiki hizo kuwa ni pamoja na Nambinzo, Bara, Iyula, Idiwili, Isalalo, Itumpi, Itaka, Hezya na Nanyala.


Mkurugenzi huyo abdallah Nandonde amewakumbusha watendaji hao kuzitunza pikipiki hizo na wafanyie kazi walizotumwa na sio vinginevyo.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, George Musyani ametoa shukurani kwa Rais Samia kwa kuwajali watendaji maana wao ndio wana kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi.


Amewataka wakatimize wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na na kukusanya mapato katika maeneo yao kwa kuwa fedha zilizonunulia pikipiki zilitokana na ukusanyaji wa mapato.



Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE