MAJAMBAZI YATEKA GARI LA MAITI SONGWE YAPORA SIMU NA FEDHA
Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limethibitisha Majambazi kuteka gari la Serikali lililokuwa limebeba maiti ya mwanafunzi katika Msitu maarufu wa Nyimbili uliopo kata ya Ntungwa tarafa ya Kamsamba Wilayani Momba.
Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe (ACP)Theopista Mallya amesema siku ya Februari 16,2023 katika misitu wa Nyimbili uliopo barabara ya Mlowo Kamsamba unaounganisha Wilaya za Momba na Mbozi mida ya saa saba na nusu usiku gari la Serikali SM 14056 likiwa limebeba maiti ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Itumbula kwenda Kijiji cha Msanyila Mbozi aliezama katika bwawa wakati anaogelea na kwenye hili gari alikuwemo Afisa Elimu wa kata ya Ivuna ambae jina lake halikutajwa na wenzie watano wakisafirisha mwili wa marehemu lakini walipofika eneo la Msitu wa Nyimbili walikuwa Magogo yamewekwa mbele yao na hapo ndio walipotekwa na Majambazi na kuporwa fedha 216,000 pamoja na simu zao vyote thamani yake ni 1,200,000 zote kwa pamoja.
Kamanda Mallya amesema Jeshi la Polisi limefanya msako na mpaka sasa watu sita wanashikiliwa na jeshi hilo huku mmoja kati yao amekutwa na simu mbili zinazodaiwa kuporwa eneo la tukio jeshi la polisi lilipomtaka kuzifungua password yake alishindwa hivyo jeshi linamuhisi hizo simu si za kwake na endapo wakibainika basi jeshi la polisi litawafungulia mashtaka Ili hatua zaidi zichukuliwe
Aidha kamanda amewataja waliokamatwa kuwa ni Shughuli Siame(47) Mkazi wa Kijiji cha Nambinzo, Furaha Sembuli(49) Mkazi wa Mlowo Wilayani Mbozi,Andalwisye Galamba(41) Mkazi wa Mtungwa Wilayani Momba
Wengine ni Oden Simtemba(45) Mkazi wa Mtungwa,Momba Lowa Simbeya(51) Makazi wa Mtungwa na Andrew Simlembe( Mkazi wa Chilulumo.
Kamanda Mallya amesema kufuatia matukio hayo mfululizo jeshi hilo la Polisi limeweka utaratibu wa Ulinzi eneo hilo masaa 24.
Ndani ya mwezi mmoja na nusu matukio ya utekaji zaidi ya matatu yametokea ndani ya msitu huo eneo hilo ambalo ni maarufu kwa jina la Bot.katika tukio la kwanza waliteka magari zaidi ya manne yakitokea mnadani na tukio la pili waliteka basi dogo la abiria aina ya coaster
Comments