MBUNGE MOMBA APENDEKEZA WAHITIMU JKT WALINDE BARABARA

 


Mbunge wa Momba, Condester Sichalwe (CCM) amependekeza Serikali kuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya mgambo kulinda barabara zisiharibiwe kwa uchafu.


Dodoma. Mbunge wa Momba Condester Sichalwe (CCM) amependekeza Serikali kuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya mgambo kulinda barabara zisiharibiwe kwa uchafu.


Sichalwe ametoa pendekezo hilo leo Ijumaa Februari 10, 2023 ndani ya Bunge alipouliza swali la nyongeza kuhusu utunzaji wa barabara ambazo zinakuwa na uchafu mwingi kutokana na wasafiri kutupa taka.


Mbunge huyo amesema wapo vijana waliomaliza Astashahada na Stashada lakini hawana kazi na hasa waliopitia mafunzo ya JKT ili wanaotupa taka watozwe faini ambazo zitatumika kuwalipa.



Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya amesema wazo la mbunge ni zuri hivyo Serikali italifanyia kazi.


"Hata hivyo niwaombe waheshimiwa wabunge na Watanzania kuwa, kutupa taka wakati unasafiri ni kosa hivyo tujitahidi kulinda na kutunza mazingira yetu kwa pamoja," amesema Kasekenya.


Akijibu swali la msingi la mbunge wa Chwaka Haji Makame Mlenge (CCM) kuhusu kuweka mazingira safi kwenye barabara zote nchini, amesema wanaendelea kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE