MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE ADAIWA KUJINYONGA

 


Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Kambarage Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani, Tatu Machemba amepoteza maisha ikielezwa kuwa amejinyonga kwa kutumia kamba chumbani nyumbani kwao Mtaa wa Mkoani mjini Kibaha, Pwani.


 Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Jumatatu Februari 20, 2023, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoani,  Shabani Rashidi amesema kuwa taarifa za tukio hilo zilimfikia juzi kwa njia ya simu na kabla ya kwenda aliwasiliana na Jeshi la Polisi.


"Nilipigiwa simu nikijukishwa tukio hilo juzi na kabla ya kwenda niliwasiliana na Jeshi la Polisi tukaenda eneo la tukio nyumbani kwa familia hiyo," amesema

Amesema kuwa baada ya kufika eneo la tukio waliingia na kukuta mwili wa mwanafunzi huyo kichwa chake kimechomekwa kwenye kamba na yeye amepiga magoti," amesema.


Mwenyekiti huyo amesema kinacholeta maswali kwa baadhi ya wananchi ni mazingira yaliyokutwa kwani mwili wa marehemu haukuwa unaning'inia bali alikutwa amepiga magoti.


"Sasa hali hiyo inawafanya watu kuwa na mshangao lakini kikubwa tunashukuru Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi na tunaamini ukweli utawekwa wazi," amesema.


Mmoja wa majirani aliyejitambulisha kwa jina moja la Monica amesema tukio la kujinyonga kwa mwanafunzi huyo limegubikwa na utata kutokana na mazingira yalivyokaa.


Monica amesema kwa sasa wanaliachia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wake kubaini sababu hasa ya mtoto huyo kujinyonga.


Naye Machite Ngonyani amesema kuwa tukio hilo linasikitisha na kuhuzunisha si tu kwa kuwa limesababisha kifo, lakini mazingira yake yana utata mkubwa.


"Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi tujue ukweli kwa kuwa mazingira ni tata kuhusu kifo cha mwanafunzi huyu,"amesema.


Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Piusi Lutumo amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa litafanyia uchunguzi zaidi.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Pwani Tumbi kwaajili ya utaratibu kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE