NYUMBA ZAIDI 30 ZAEZULIWA NA MVUA YENYE UPEPO MKALI


 Licha ya makazi ya watu pia mvua hiyo imeharibu madarasa mawili  na vyoo vya shule Sekondari Kiva.

Handeni. Nyumba zaidi ya 30, madarasa mawili na vyoo vimeezuliwa na mvua wilayani Handeni mkoani Tanga katika mvua zilizonyesha zikiambaytana  na upepo Februari saba


Wakizungumza kwenye ziara ya kamati ya siasa ya kukagua maeneo ambayo yameathiriwa na mvua hizo ,baadhi ya waathirika wamesema upepo ulikuwa ni mkali kiasi cha watu kutosikilizana.


Mkazi wa Mbwagwi Mwanahamisi Ally amesema kuwa baada ya kuona upepo huo ni mkali sana,aliwaambiwa watoto waliopo ndani wasikimbka na kuwakumbatia ambapo nyumba iliezuliwa bati.


Aidha Shabani Yusuph ameshauri wadau kujitokeza kwa kusaidiana na serikali kwenda kuwasaidia chakula kwani wengine hata vyakula vimeharibika.


"Vyakula ambavyo tulihifadhi kama akiba pia vimeharibika hivyo wadau kwa kushirikiana na serikali walione hili,na kuja kutusaidia huku mkikumbuka wakati huu hali ni mbaya",ameswma


Diwani kata ya Kiva Valentino Mbuji amesema kwa eneo hilo kuna waathirika 19 ambao nyumba zao zimeathirika,hivyo wanahitaji msaada.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Handeni Amiri Changogo amesema tathimini imeshafanyika hivyo utaratibu wa kuwasaidia waathirika muda wowote utafanyika.


"Nyumba zaidi ya 30 zimeezuliwa pamoja na taasisi za serikali hivyo wananchi na  wanafunzi wameathirika, wadau wasiachie Serikali pekee katika hili wote tujitokeze na kuwasaidia wenzetu", amesema Changogo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE