WANANCHI ILEJE WAMKATAA MWENYEKITI WA KIJIJI

Wananchi wa kijiji cha Shinji kata ya Mbebe wilayani Ileje mkoani Songwe wamesema hawana Imani na mwenyekiti wa kijiji hicho Ali  Kalinga akishutumiwa kuwamilikisha baadhi ya wananchi wakiwepo ndugu zake eneo lililotengwa na wananchi kwa ajili ya matumizi ya malisho Zaidi ya hekari 50.


Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Kaimu afisa Tarafa ya Bulambya Frank Mwampamba ambaye alimwakilisha mkuu was wilaya hiyo Farida Mgomi walisema mwenyekiti huyo alihusika kugawa maeneo hayo bila kushirikisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji na wananchi waliopitisha kutenga eneo hilo tangu miaka ya nyuma.


Lingisoni Sikanyika mkazi wa kijiji hicho alisema mwenyekiti huyo alitumia madaraka yake kuwagawia kwa nguvu baadi ya ndugu zake na kushindwa kuwaondoa wananchi wengine waliovamia eneo Hilo  Zaidi ya hekari 20.


Sikanyika alisema mwenyekiti wetu atupishe kwenye kiti tumeshindwa kuendelea kufanya naye kazi kwani yeye yupo mbele kuharibu matumizi bora ya mpango aridhi ya kijiji ambayo wananchi walikubalina kupitia mkutano wa hadhara tutenga kwa ajili ya malisho na kuwagawia baadhi ya vijana wa kijiji hicho ambao watakuwa na uhitaji wa aridhi kwa ajili ya kulima na kujenga.


Fikisoni Mwamlima alisema tangu amezaliwa kijijini hapo anamiaka 63 wazee hao wamekuwa na utamaduni wa kulinda maeneo hayo hivyo mwenyekiti ambaye walimchagua mwaka 2020 ameharibu utaratibu wa mpango wa matumizi ya aridhi ambayo ni ajenda ya kila kijiji kutenga maeneo hivyo mwenyekiti huyo amekiuka utaratibu hivyo aondoke ili wachague mwingine.


“Mwenyekiti amekuwa akigawa maeneo kama njugu hususani kwa ndugu zake na wengine ambao wanampa hela hali ambayo imepelekea kuhujumu kijiji na nikuombe afisa tarafa kwaniaba ya mkuu wa wilaya ondoka naye hatutaki atuongoze”, alisema Mwamlima.


Mwenyekiti wa kijiji hicho Ali Kalinga alisema hahusiki na tuhuma hizo bali anatambua eneo hilo kuvamiwa lakini alimwagiza mtendaji wa kijiji hcho kuwashughulika waliovamia eneo lililotengwa licha ya kukiri baadhi maeneo waligawa na mtendaji bila kuwataarifu wananchi.


Diwani wa kata hiyo John Katofani Mtafya alisema chuki ya wananchi kwa mwenyekiti huyo  imetokana na kugawa maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya kijiji bila kuwashirikisha wananchi ambao walitenga maeneo hayo ambayo walitoa wengine kutoka kwa babu zao lakini leo wanashangaa maeneo kumilikiwa na watu.


Kaimu afisa Tarafa ya Bulambya Frank Mwampamba alisema wanakijiji wanapaswa kuzisimamia Serikali zao za vijiji ili ardhi yao isichukuliwe bila kufuata utaratibu kwani kuna baadhi ya sehemu baadhi ya viongozi wamekuwa sio waaminifu wanagawa ardhi ya kijiji bila kuwashirikisha wenye ardhi yao.


“Mimi sitaamua kumtoa mwenyekiti wa kijiji bali napeleka malalamiko yeno kwa mkuu wa wilaya na yeye atakuja kutoa maamuzi ya hili tatizo na niagize maaeneo hayo yasitishwe kulimwa mpaka suluhu itakapopatika ikiwepo kurudishwa mikononi mwa wananchi mpaka watakapobadilisha matumizi”, alisema Mwampamba.


 Mwampamba aliongeza kuwa kijiji kinatakiwa kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwani itaondoa migogoro ya mipaka mbalimbali vilevile ni chombo kinachoonesha ni kiasi gani cha ardhi kilichopo kwa ajili ya shughuli za kijiji kama mifugo, kilimo, makazi, viwanda pamoja na matumizi mengine.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE