SENEDA AWAONYA WANAOWABEZA WALIMU SONGWE, ILEJE YAWAPONGEZA WAALIMU KWA KUWAFANYIA SHEREHE

 

Wakuu wa Idara ya elimu msingi na sekondari katika halmashauri za mkoa wa Songwe wameonywa kujiepusha na tabia ya kutoa kauli zisizofaa Kwa walimu  pindi wanapowasilisha changamoto zinazowakababili bali wajenge daraja litakalosaidia kuoandisha kiwango Cha ufaulu.

       ( Katibu Tawala Seneda katikati kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe akicheza Muziki pamoja na Waalimu)


Hayo yamesemwa na katibu Tawala mkoa wa Songwe Happiness Seneda wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule zilizofanya vizuri Kwa matokeo ya darasa la Saba 2022 wilayani Ileje ikiambatana na kutoa vyeti vya pongeza ,fedha , na majiko ya gesi Kwa shule zilizopo katika mazingira magumu.


Hafla hiyo imefanyika Februari 4, 2023 katika ukumbi wa RM  Itumba ikiandaliwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kwa lengo la kuendeleza ufaulu ambao umepanda kutoka 56% mpaka 65% 

       ( Afisa Elimu Mkoa wa Songwe)


Happiness amesema mkoa wa Songwe upo katika mikakati ya kuongeza kiwango Cha ufaulu hivyo kauli mbovu Kwa walimu kumekuwa chanzo Cha kushusha morali Kwa walimu ambao wamejitolea kufanya kazi katika mazingira magumu.


Seneda amezinyoshea vidole ofisi za masijala kuwa vinara wa kukwamisha michakato ya barua za walimu huku akiwataka wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Songwe kutoa mafunzo elekezi Kwa watumishi wa masijala Ili wafanye kazi Kwa weledi walionao.


"Masijala ni nani katika ofisi zetu wawanyanyase watumishi wengine lakini sio walimu nikibaini hilo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao", amesema Seneda.


Afisa elimu mkoani humo Michael Ligola amesema hafla ya kuwapongeza walimu na shule zilizofanya vizuri imeonyesha matunda ya kuelekeza kuirudisha Ileje ya miaka ya 2000 katika kufaulisha huku akizitaka halmashauri zingine kuiga.

        ( Waalimu wakimsikiliza kwa Makini Katibu Tawala Seneda)


Alisema mkoa wa Songwe bado haufanyi vizuri katika ufaulu wa matokeo ya darasa la Saba, Kwani matokeo ya msimu wa masomo wa 2022 ulishika nafasi ya 20 kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara.


Amesema wamejikita kuimalisha elimu ya awali na darasa la kwanza Ili watoto wapate Msingi mzuri ambapo watamudu vizuri katika stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi amesema ataendelea kutoa ushirikiano kwa walimu ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zao mapema.


Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Ileje Geofrey Mnauye amesema shule ambazo zipo mbali na miundo mbinu kusumbua kutokana na muundo wa Wilaya Hiyo, amesema atakuwa karibu zaidi na walimu hao na kutatua changamoto zao mapema Ili kuwaongezea nguvu ya kujitolea zaidi kufundisha watoto.


Mnauye amesema lengo lao nikifika ufaulu wa asilimia 75 kwa matokeo ya mwaka huu wa masomo wa 2023.


Ikumbukwe kuwa wilaya ya Ileje imewahi kushika nafasi ya kwanza kimkoa mwaka 2000 na kuanzia hapo ilianza kushuka kitaaluma, na kupelekea mwaka 2022 mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuanzisha motisha Kwa walimu na shule zitakazofanya vizuri ambapo hapo Jana vyeti vimetolewa Kwa shule zilizoongoza kiwilaya.

Katika hatua nyingi Mkurugenzi aliwakabidhi kupitia Katibu Tawala Majiko ya gesi shule zilizopo katika mazingira Magumu.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE