WATUMISHI NA WAZABUNI 672 MIKONONI MWA TAKUKURU

 


Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angela Kairuki amesema watumishi na wazabuni 672 wamefanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) huku akidai wameanza kuwachukulia hatua waliotajwa na CAG.


 Kairuki ameyasema hayo leo Februari 7,2023 wakati akichangia taarifa ya utekezaji wa shughuli za kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).


Amesema kuwa wameshaanza kuchukua hatua kwa watumishi waliotajwa katika ripoti ya CAG kupitia sektarieti za mikoa na Takukuru.


Amesema wamepata mrejesho kutoka kwa Mkurugenzi wa Takukuru kuwa watumishi na wazabuni 672 wameshafanyiwa uchunguzi na taasisi hiyo.


“Wazabuni na watumishi 46 uchunguzi umeshakamilika kutokana na kutodhibitika kwa tuhuma zao lakini watumishi na wazabuni 53 majalada yao yako kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kuomba kibali wafikishwe mahakamani,”amesema Kairuki.


Amesema watumishi na wazabuni 51 mashtaka yao yako mahakamani na kuwa yote yaliyosemwa na wabunge watayachukua na wataendelea kuchukua hatua kwa wote watakaodhibitika kufanya ubadhilifu.


Amesema hawatafumbia macho kwa watu wote watakaobainika kufanya ubadhilifu katika fedha za umma.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE