WAZIRI MKUU AKOSHWA NA MWEKEZAJI KIJANA KIWANDA CHA KAHAWA SONGWE
WAZIRI Mkuu Kassim Majiliwa amekoshwa na uwekezaji mkubwa wa kiwanda kikubwa Cha kahawa Cha GDM kinachoendeshwa na kijana mzawa Richard Mwangoka mwenye umri wa miaka 22 kinachochakata kahawa iliyonunuliwa kwa wakulima wazawa.
Akiwa katika Ziara ya Siku tatu katika mkoa wa Songwe , akitembelea kiwanda na kuongea na wafanyajazi wa kiwanda Cha GDM alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Dokta Samia Suluhu Hassani inafurahishwa na uwekezaji mkubwa unaofanywa na kijana mzawa ambaye anatengeneza ajira , biashara na uchumi.
Alisema zao la kahawa ni miongoni mwa mazao makuu ya kimkakati ndani ya Nchi yetu ambalo Serikali inatoa kipaumbele kutokana na kukuza uchumi wa Wananchi na Taifa .
"Rais wetu Dokta Samia Suluhu Hassan anahamasisha sana wawekezaji wa ndani, Leo hii nimefarajika sana kwa kupata mwekezaji kijana mzawa ambaye anatengeneza ajira, kukuza soko kwa kuliongezea thamani kwa kulichakata zao la kahawa na kukuza uchumi wa Wananchi na Taifa
Pamoja na baba yake aliyeanzisha kiwanda hiki kufariki , kijana huyu ameendelea kuyabeba maono ya baba yake na na kuendeleza kiwanda hiki kikubwa" alieleza Waziri Mkuu.
Amevisisitiza vyama vya wakulima
AMCOS kuuza kahawa yao kwa kiwanda hicho Cha GDM cheny uwezo wa kununua kahawa kwa wingi na kuichakata kwa ajili ya kuuza nje ya Nchi.
Pia amemuagiza mratibu wa TARURA Wilaya ya Mbozi kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu ya barabara kwenye kiwanda hicho Cha mwekezaji mzawa Ili bara bara ipitike msimu wote.
Alisema ni muhimu wawekezaji wazawa kupewa kipaumbele kama walivyo wawekezaji kutoka nje Ili kuwajengea Mazingira mazuri ya kuboresha Biashara.
Kuhusu makato yaliyopo kwenye zao la kahawa Waziri Mkuu alisema wanaendelea kupitia mikoa yote inayozalisha zao la kahawa Ili kupunguza makato mengi ambayo yanashusha tija kwa wakulima.
"Tayari tumepita mkoa wa Kagera, mkoa wa ruvuma na Kilimanjaro tayari tumepunguza kwa kiasi kikubwa makato kutoka 40 na kubakia matano, Tunakuja Songwe tutahakikisha makato hayazidi matano" alisema Wazir Mkuu.
Mkurugenzi wa kiwanda Cha GDM Richard Mwangoka anayesimamia kiwanda hicho kikubwa baada ya baba yake Gervas Mwangoka kufariki alisema Kiwanda hicho kilicho anzishwa mwaka 2008 kimeajili wafanya Kazi 80 wanaofanya Kazi kiwandani.
Alisema kwa upande wa wafanya Kazi wanaofanya Kazi za vibarua ni zaidi ya 200 huku wafanyajazi wanaofanya Kazi za shambani wakiwa zaidi ya 40.
Mwangoka alisema mpaka sasa kiwanda hicho Kinakusanya Tani 500 za kahawa kutoka kwa wakulima , ambazo huuzwa nje na nyingine kuchakatwa kwa ajili ya kutumika katika unywaji wa ndani
" Pamoja na kukoboa kahawa pia Tumejikita zaidi kuchakata kahawa ya kunywa Ili kuongeza na kukuza soko la ndani ambalo Lina faida kubwa tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya kahawa huuzwa nje ya Nchi.
Pia tunajipanga kuongeza ununuzi wa kahawa kutokana na kiwanda chetu kuhitaji mzigo mkubwa zaidi" alisema Mwangoka.
Kwa upande wa Mbunge Mbozi George Mwenisongole alisema kuwa wakulima wengi wa zao la kahawa wanaumizwa kwa kiasi kikubwa Cha makato mengi yaliyopo kwenye zao Hilo .
Alisema haiwezekani makato ya wakulima wa Songwe yatofautiane na makato ya wakulima wa Kagera , Kilimanjaro na Ruvuma wakati zao Hilo ni moja.
Comments