WAZIRI MKUU MAJALIWA KUANZA ZIARA MKOANI SONGWE JUMATATU
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Songwe ya siku 3 kuanzia tarehe Februari 13,2023 na kuhitimisha Februari 15,2023 ambapo atafanya Halmashauri zote sita za Mkoa wa Songwe.
Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba amesema Mkoa wa Songwe tunatarajia kumpokea siku ya tarehe 13,2023 na ataanza ziara katika Wilaya ya Songwe ambapo ataweka jiwe la msingi hospitali ya Wilaya iliopo eneo la kaloreni pia ataongea na Wananchi baada ya hapoo Waziri Mkuu ataongea na Watumishi wa Wilaya ya Songwe katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Mwambani.
Kindamba amesema siku inayofuatia ya tarehe Februari 14,2023 Waziri Mkuu atatembelea kiwanda cha Mwekezaji Gdm kilichopo Mlowo na kisha ataelekea makao makuu ya Wilaya ya Momba Chitete ambapo atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kukagua soko la Kimataifa la Kakozi kisha siku hiyo hiyo ataelekea Halmashauri ya Tunduma ambapo Waziri Mkuu ataongea na Wananchi wa Tunduma eneo la kastamu pia atazindua madarasa 10 ya shule ya Msingi Haisoja ambapo pia atazungumza na Wananchi.
Aidha siku ya Februari 15 Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi hospitali ya Mkoa wa Songwe na ataongea na Wananchi kisha ataelekea Wilayani Ileje siku hiyo hiyo ambapo atakagua shule ya Wasichana ya Ileje pia atakagua jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) hospitali ya Wilaya ya Ileje ambapo pia ataongea na Wananchi.Mara baada ya kutoka hapo Waziri Mkuu atarejea Makao makuu ya Mkoa kwa maana ya Mbozi ambapo ataongea na Watumishi wote Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa ambapo pia atafanya majumuisho ya Ziara yake.
"Niwaombe Wananchi wa Songwe wajitokeze kwa wingi na kwa utulivu bila kusahau kuwa makini na misafara wasikatize katize ovyo barabarani lakini pia niwahakikishie maeneo yote yapo salama kwani tumeimalisha Ulinzi na Songwe ni salama Wananchi wajitokeze" amesema Kindamba
Comments