WEZI WAVAMIA NYUMBANI KWA KAMANDA WA POLISI WAIBA BUNDUKI
Wezi katika kaunti ya Busia walivaamia nyumbani kwa kamanda huyo usiku wa manane na kuiba bunduki aina ya Czeska, polisi wameanza upelelezi wa tukio hilo.
Kenya. Polisi katika kaunti ya Busia wameanza msako kutafuta bastola aina ya Czeska iliyoibwa kwenye nyumba ya kamanda wa polisi wa kaunti hiyo usiku wa Jumamosi, Februari 18 ambapo wezi mbali na bastola waliiba redio na mtungi wa gesi.
Inasadikika wezi hao walinyunyiza dawa ya kulewesha kupitia dirisha la chumba alichokuwa amelala kamanda huyo kabla ya kutekeleza tukio lao kkitu ambacho kilimsababishia maumivu ya kichwa na kupata kiznguzungu alipoamka.
Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo ya Busia, Bishar Muhumed SSP amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa jana na wezi hao walipora vitu ikiwemo bastola anayomiliki kamanda huyo.
Maofisa wa usalama wametembelea eneo la tukio na kikosi cha wapelelezi wakiwa na mbwa wa kundi la K9 kwa ajili ya kuchukua harufu ambapo aliwapeleka barabara inayokwenda Uganda lakini huyo alipoteza dira kabla ya kufika mpakani mwa nchi hizo.
Taarifa zaidi zinasema hakuna aliyekamatwa au kupatikana hadi sasa, licha ya juhudi za upelelezi zinazoendelea.
Hili ni tukio la pili mfululizo la hivi karibuni la kuibwa kwa bunduki nchini kenya ambapo Ofisa mmoja wa Polisi OCPD mjini Narok alitekwa nyara na watu wasiojulikana kwenye lango la nyumba yake alipokuwa akirejea nyumbani na kumporwa bastola aina ya Jericho ikiwa na risasi 14 kisha kumtelekeza afisa huyo msituni.
Comments