BARABARA YA ISOKO-KATENGELE KUJENGWA KWA ZEGE

Kutokana na Barabara ya Isoko-Katengele kuwa na miinuko mikali pamoja na kona kali zipatazo 62, Wakala wa Barabara za vijijini na mjini (TARURA) imeanza kujenga Barabara hiyo kwa kutumia zege kwa sehemu zote ambazo zina kona kali na miinuko ili kurahisisha mawasiliano kwa watumiaji wa Barabara haswa wakazi wa Kata ya Kafule, Sange, Ibaba, Ngulugulu na lubanda ambao wamekuwa wakipata adha kipindi cha mvua kwenda katika Hospitali kongwe ya Isoko ambayo imejengwa enzi za ukoloni 1889 pamoja na kusafirisha mazao yao.

 


Meneja wa TARURA Wilaya ya Ileje, Mhandisi Lugano Mwambingu amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamilia  kwa dhati kuwaondolea changamoto ya mawasiliano wananchi wanaotumia Barabara kwa kutoa fedha za matengenezo milioni 649, 882,000.


Mhandisi Mwambingu amesema kazi nyingine zinazofanyika ni pamoja na kukata magema ya Barabara kwa ajili ya utanuzi wa Barabara, kujenga gabion na kuumba tuta kazi zote zinaendelea.


"Kwa kuzingatia umhimu wa barabara hii TARURA itaendelea kuipangia fedha za matengenezo kila mwaka ili kuimalisha iweze kupitika kwa mwaka mzima" amesisitiza  Mhandisi Lugano Mwambingu.

Wenicom Mbembela mkazi wa Ileje Kijiji cha Shikunga (72) ameishukuru Serikali kwa ukarabati wa Barabara ya Isoko-Katengele ambao utakwenda kuondoa utelezi uliowasumbua kwa muda mrefu ukizingatia Barabara hiyo inawaunganisha na huduma ya kijamii Hospitalia ya Isoko pamoja na usafirishaji wa mazao na mbao.


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE