HIZI HAPA BARABARA ZILIZOPENDEKEZWA KUPANDISHWA HADHI MKOANI SONGWE

 Kikao cha bodi ya barabara Mkoani Songwe kikiongozwa na Mwenyekiti ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Francis Michael kilichofanyika jana 06 machi 2023 katika ukumbi mdogo Mkuu wa Mkoa wa Songwe kimependekeza na kupitisha mapendekezo ya  baadhi ya barabara kupandishwa hadhi na kuanza kuhudumiwa na Wakala wa barabara tanroads badala ya Tarura.

Katika kikaoa hicho kilichohudhuliwa pia na Mbunge wa Ileje ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Songwe Radwell Mwampashe, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa taasisi na Wajumbe toka taasisi mbali mbali kwa pamoja walilidhia hoja ya kuzipandisha hadhi barabara 6 ambapo kabla ya kufunga hoja Mkuu wa Wilaya ya Songwe Solomoni Itanda aliomba barabara mbili toka Wilayani Songwe zipandishwe hadhi hiyo lakini kikao kiliazimia barabara moja ya Kininga-ngwala  ndio iingizwe kwenye mpango huo na nyingine iletwe kikao kijacho.


Hizi hapa barabara zilizopitishwa


Itumbula-Namkukwe-Galula(Momba-Songwe


Galula-Itindi-Magamba( Songwe-Mbozi)


Ihanda -Ipunga(Mbozi)


Isoko- Katengele(Ileje)


Ibaba-Katengele(Ileje)


Ikana-Makamba(Momba)


Kininga-Ngwala(Songwe)

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE