DC ILEJE AZIASA AMCOS KUJENGA UAMINIFU KWA WAKULIMA WA KAHAWA
Wakati wilaya ya Ileje mkoani Songwe ikipambana kutengeneza mazingira rafiki Kwa wakulima wa mazao ya kimkakati ikiwepo Kahawa, Pareto, Iriki na mengine vyama vya ushirika vimeaswa kujenga uaminifu Kwa wakulima.
Wito huo umetolewa Machi 8,2023 na mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi wakati wa kikao Cha wadau wa kahawa kilichowakutanisha wakulima, viongozi wa Amcos na baadhi ya makampuni yanayonunuza zao la kahawa kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri Ileje.
Mgomi amesema viongozi wa AMCOS wanapaswa kusimamia maslahi ya wakulima wa Kahawa kuwapa fedha zao kwa wakati ili wakulima waongeze wigo wa kulima zao hilo.
"Mazao yanunuliwe kupitia vyama vya ushirika Kwa mujibu wa Sheria na hairuhusiwi mtu yeyote kununua anavyotaka yeye kwa kuwarubuni wakulima na kuwadhulumu fedha zao", amesema Mgomi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ileje Geodfrey Mnauye amesema ili kuongeza uzalishaji wa kahawa wazalishaji wa mbegu hiyo TACRI wanapaswa kuzalisha mbegu kwa wingi na yenye ubora kuendana na mazingira ya ukanda wa Bundali.
"Kutokana na elimu ya kilimo bora Cha kahawa wakulima wanapaswa kuitumia na kuwataka vijana kuhamasika kujiingiza kulima zao hilo kwani kahawa ya Ileje ni bora hii inatokana na uwanda inakolimwa,elimu na kanuni za kilimo bora",amesema Mnauye.
Afisa kilimo wa halmashauri hiyo Herman Njeje amesema ili kuboresha kilimo wilayani humo wanatarajia kugawa pikipiki 29 kwa maafisa ugani ili kuhakikisha wanafikisha elimu ya kilimo bora kwa wakulima.
"Katika kuzalisha zao la kahawa tumekuwa tulipanda Kila mwaka ambapo kwa mwaka 2022 tumezaliza zaidi ya tani 1000 hivyo kwa mwaka 2023 tunatarajia kuzalisha kwa wingi na kuwavutia wawekezaji watakaonunua zao hilo Kwa wakati", amesema Njeje.
Joshua Kalonge katibu wa AMCOS kata ya Lubanda wilayani humor amesisitiza kuwa viongozi wa Amcos wahakikishe wanafuatilia ubora wa kahawa kutoka hatua ya mkulima mpaka kiwandani na kuwataka wakulima kutumia elimu ya kitaalamu kuandaa kahawa iliyo bora zaidi.
Wilaya ya Ileje imekuwa ikijihusisha na baadhi kilimo Cha mazao Pareto, Kahawa, Iriki ,Tangawizi Kwa ukanda wa Bundali na Kwa ukanda wa Bulambya hujihusisha na kilimo Cha Mahindi, karanga, Ulezi na alizeti hivyo katika kuimarisha na kuendeleza uzalisha kiwango Cha juu wananchi Kwa kushirikiana na wataalamu wanapaswa kutumia mbinu za kitaalamu kupata mazo mengi yaliyo bora.
Comments