MBOZI NA MOMBA ZAPATA HATI SAFI RIPOTI YA CAG

Halmashauri za Mbozi na Momba zilizopo Mkoani Songwe ni miongoni mwa halmashauri zilipopata hati safi huku Halmashauri ya Songwe ikiwa ni halmashauri pekee iliopata hata yenye mashaka kulingana na ripoti ya CAG.


Rais wa Dkt Samia Hassan amewataka Viongozi na Watendaji wa serikali kuzisoma na kuzielewa vyema taarifa za rushwa na za ukaguzi wa hesabu za serikali ili ziwasaidie kujitathimini.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAG Halmashauri  za Mbozi,Momba, Tunduma na Ileje zimefanikiwa kupata hati safi huku Halmashauri ya Songwe ikiambulia hati yenye mashaka na kuwa ni halmashauri moja tu katika Mkoa wa Songwe yenye hati yenye mashaka.


Wakiongea kwa nyakati tofauti juu ya mapokeo ya hati hizo baadhi ya wakurugenzi wamewashukuru Madiwani na Watumishi wa halmashauri zao pamoja na Wananchi.

"Kiukweli sisi Mbozi tumefarijika sana kwa hii hati tuliopata na kwa upande wangu binafsi hii ni hati yangu ya kwanza kupata toka nimeletwa kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbozi lakini hizi sio juhudi zangu binafsi bali ni ushirikiano tulionao ndani ya halmashauri yetu ya Mbozi" Abdallah Nandonde Mkurugenzi Mbozi



Nae Mkurugenzi wa halmashauri ya Momba Regna Bieda amesema amefarijika sana kwa hati hiyo na huo ni ushindi mkubwa kwa Wanamomba na itawafanya kuongeza juhudi zaidi katika ukusanyaji wa mapato na matumizi sahihi ya fedha za Serikali.


"Niwapongeze kwa kweli Viongozi na Watendaji wote wa Halmashauri ya Momba kwa kuchapa kazi kwa pamoja huu ni ushindi wetu sote" Regna Bieda Mkurugenzi Momba

 Nawe Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbozi George Mushani ameipokea hati hiyo kama ushindi katika Wilaya yake na chachu ya kuendelea kufanya vizuri katika ripoti zingine za CAG. 

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE